Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

1 1 8 /

U O N G O F U & W I T O

C. Hatupaswi kutumia uhuru wetu kama kibali au kifuniko cha dhambi, bali kama fursa ya kutimiza Amri Kuu, yaani, kuwapenda na kuwajali wengine.

1. Petro anatuhimiza tusitumie uhuru wetu kama kifuniko cha uovu, bali tuishi kama watumishi wa Mungu, 1 Pet. 2:16.

2. Tumia uhuru wako kama fursa ya kuonyesha upendo kwa watu wote, lakini hasa wale wa jamii ya imani, Gal. 5:13.

3. Mungu anaturuhusu tuwe huru ili tuwapende wengine.

a. Tunapaswa kuwa mambo yote kwa watu wote ili kuwaokoa, 1 Kor. 9:19-23.

b. Tuko huru kutumia chochote ambacho hakiko nje ya mapenzi ya Mungu ili kuwavuta wengine kwake, 1 Kor. 3:21-23.

4

D. Madhumuni ambayo tumeitiwa kutumia uhuru wetu katika Kristo.

1. Kwa mambo yafaayo, 1 Kor. 6:12a – Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo.

2. Si kwa kitu chochote ambacho ni cha kudhuru na cha kulevya, 1 Kor. 6.12b – vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu cho chote.

3. Kwa yale tu yenye kujenga, 1 Kor. 10:23 – Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vijengavyo.

Made with FlippingBook flipbook maker