Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
/ 1 1 7
U O N G O F U & W I T O
c. Haki ya Sheria inatimizwa ndani yetu, sio na sisi wenyewe, kwa Roho Mtakatifu.
2. Tumewekwa huru kutokana na juhudi tupu za matendo mafu ili kumpendeza Mungu kwa ustahili na nguvu zetu wenyewe.
a. Tunaokolewa kwa neema kwa njia ya imani, si kwa matendo, Efe. 2:8-9.
b. Kilichosalia sasa kwa watoto wa Mungu ni pumziko, kwamba sasa wanaweza kuachana na kazi zao zilizokufa ili kumtumikia Mungu katika ukweli, Ebr. 4:9-10.
c. Dhamiri zetu sasa zimesafishwa na kutakaswa kwa sababu ya damu ya Kristo na kukubalika kwake na Mungu akiwa msalabani, Ebr. 9:13-14.
4
3. Tumewekwa huru mbali na udhalimu wa shetani, hasa ukandamizaji wake kupitia hofu ya kifo, Ebr. 2:14-15.
a. Kwa njia ya msalaba, Kristo amefanya onyesho la wazi la enzi na mamlaka (Kol. 2:15).
b. Adui hawezi kutuangamiza au kutukandamiza ikiwa tutasimama imara katika ushindi alioupata Kristo kwa ajili yetu. (1) Yakobo 4:7
(2) 1 Yohana 4:4 (3) 1 Petro 5:8-9
Made with FlippingBook flipbook maker