Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

1 1 6 /

U O N G O F U & W I T O

II. Neno Linatuita kwenye Uhuru katika Kristo kama Fursa ya Kutimiza Amri Kuu, na kwa Kusudi la Kuwaokoa Wengine kwa Njia ya Kristo.

ukurasa 203  9

A. Kwa sababu ya kazi toshelevu ya Yesu Kristo msalabani, Mungu anawaita wanafunzi wake wote kuishi maisha ya uhuru katika Kristo.

1. Yesu alishinda kwa kusudi la kuleta uhuru, na hatupaswi tena kunaswa katika nira yoyote ya utumwa.

a. Kristo ametuweka huru kupitia kifo chake msalabani, Gal. 5:1.

b. Tumeitwa kwenye uhuru, Gal. 5:13.

2. Kupitia damu ya Yesu, tumekombolewa kutoka katika kila namna ya kujihesabia haki na utumwa wa dhambi (Yohana 8:31-36).

4

3. Kwa njia ya imani katika Kristo tumempokea Roho Mtakatifu ambaye ametufanya wahudumu wa agano jipya, 2 Kor. 3:17.

B. Viwango na vipengele vya uhuru tulionao katika Kristo.

1. Tumewekwa huru mbali na hatia na hukumu ya Sheria, Rum. 8:1-4.

a. Katika Yesu Kristo tumewekwa huru mbali na hukumu zote.

b. Kwa sababu ya asili ya mwili, haki kwa njia ya kutimiza Sheria haiwezekani.

Made with FlippingBook flipbook maker