Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
/ 1 1 5
U O N G O F U & W I T O
2. Tumempokea Roho Mtakatifu, ambaye anaitwa “Roho wa kufanywa wana” Rum. 8:15-16.
3. Roho wa kufanywa wana ametufanya kuwa watu wa Mungu, watoto wake, na wanawe, warithi wa Mungu katika Kristo, Rum. 8:15-16.
C. Wito huu kwenye jumuiya kwa njia ya kuzaliwa upya na kuasiliwa una madokezo kadhaa ya kiutendaji kwetu sisi kama Wakristo na viongozi wa Kanisa:
1. Mungu anatuita tuishi katika jumuiya, si kwa kujitenga.
2. Tumekuwa washirika wa Kanisa moja la kweli la mahali pote na nyakati zote.
3. Ufuasi wa kweli unahusisha kuwa katika ushirika wa waamini wa mahali pamoja.
4
4. Uongozi wa Kikristo ni kwa ajili ya kulijenga na kulitia nguvu Kanisa ili liwe yote ambayo limeitwa kuwa katika Yesu Kristo, Ebr. 13:17.
5. Wito wa kukua na kufikia ukomavu katika Kristo ni wito kwa jumuiya, si tu wito kwa ustawi wangu binafsi unaowatenga wanafunzi wengine.
Made with FlippingBook flipbook maker