Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
1 1 4 /
U O N G O F U & W I T O
b. Bila kujali asili yetu, hali, au historia ya kijamii, kupitia imani katika Kristo tumekuwa kitu kimoja katika Yesu Kristo.
(1) Wagalatia 3:28 (2) Wakolosai 3:11
3. Waamini wamepata kuoshwa kwa kuzaliwa upya na kufanywa upya kwa Roho Mtakatifu (yaani, sasa wanashiriki nasaba (DNA) ya Mungu ya kiroho kupitia Yesu Kristo), Tito 3:5-6.
4. Kwa njia ya Roho Mtakatifu, tumeunganishwa na uzima wa Mungu katika Kristo, na kushiriki pamoja katika maisha yale ya kweli yanayowajaza watu wa Mungu.
a. 1 Kor. 12:13
b. Efe. 1:13
4
c. Kuna mwili mmoja na imani moja tu, na tumaini moja tu la wito wetu, Efe. 4:4-6.
d. Maisha ya Kikristo ni maisha ya kijumuiya, maisha yanayozaliwa, kukulia na kukomaa katika muktadha wa jumuiya ya Kikristo.
B. Kupitia kuzaliwa upya, Mungu hutuweka katika jumuiya yake kwa njia ya kufanywa wana kiroho.
1. Tumeasiliwa katika familia ya Mungu kwa imani: huiothesia - «kuweka» (mchanganyiko wa neno la Kiyunani linalomaanisha «mwana» na kitenzi «kuweka»).
Made with FlippingBook flipbook maker