Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

/ 1 1 3

U O N G O F U & W I T O

• Kama washirika huru wa watu wa Mungu ( laos ), tumeitwa kufanya utume. Sisi kama wanafunzi wa Yesu wa karne ya 21, tumeitwa kutimiza Agizo Kuu, la kufanya mataifa yote kuwa wanafunzi, kupigana vita na adui yetu wa kiroho ibilisi, na kudhihirisha maisha ya Ufalme kupitia upendo na matendo yetu mema.

I. Neno la Mungu Linaloita Hakika Linatuita Kuishi na Kufanya Kazi Katika Jumuiya, kama Washirika wa familia Yake, Tukiishi Hadithi ya Mungu kama Watu Wake ( Laos ya Mungu).

Muhtasari wa Sehemu ya 2 ya Video

ukurasa 202  8

A. Neno la Mungu linalotuita kwenye jumuiya hutufanya tushiriki maisha halisi ya Mungu kupitia kuzaliwa upya.

1. Palingenesia – uongofu na “kuzaliwa upya.” Nguvu ya Neno la Mungu kwa kweli inaumba ndani yetu maisha halisi ya Mungu, tunaunganishwa na maisha ya Mungu mwenyewe.

4

a. Sasa tumekuwa washiriki wa asili ya uungu ya Mungu, tukishiriki uzima wake mwenyewe, 2 Pet. 1:3-4.

b. Sisi ni washirika wa watu wa Mungu na familia yake, 1 Yohana 3:1.

c. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; kilichozaliwa kwa Roho (yaani, kwa uzima wa Mungu mwenyewe) ni roho, Yohana 3:5-6.

2. Waamini wameunganishwa pamoja kama kitu kimoja katika maisha ya Yesu Kristo.

a. Sasa tuko “ndani ya Kristo” ambaye anakuwa chanzo chetu na uhai wetu (Kol. 3:4).

Made with FlippingBook flipbook maker