Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
/ 1 6 7
U O N G O F U & W I T O
Ushauri Mtaala wa Capstone
• Kwanza, soma kwa makini utangulizi wa Moduli kwenye ukurasa wa 5, na uvinjari mwongozo wa Mkufunzi ili kupata uelewa wa maudhui ambayo yatashughulikiwa katika kozi. Kitabu cha Kazi cha Mwanafunzi kinafanana na Mwongozo wa Mkufunzi wako. Mwongozo wako, hata hivyo, pia una sehemu ya nyenzo za ziada kwa kila somo, inayoitwa Maelezo ya Mshauri. Marejeo ya maelekezo haya yanaonyeshwa kwenye ukingo kwa ishara: . Majaribio, Mtihani wa Mwisho, na Funguo za Majibu zote zinaweza kupatikana kwenye Satelaiti ya TUMI. (Hii inapatikana kwa satelaiti zote zilizoidhinishwa.) • Pili, unahimizwa sana kutazama mafundisho kwenye DVD zote mbili kabla ya kuanza kwa kozi. • Tatu, unapaswa kusoma masomo yoyote uliyopewa yanayohusiana na mtaala, iwe vitabu vya kiada, makala au viambatanisho. • Nne, inaweza kusaidia kupitia mada kuu za kitheolojia zinazohusiana na kozi kwa kutumia kamusi za Biblia, kamusi za kitheolojia, na fafanuzi za Biblia ili kuchochea uzoefu wako na mada kuu zinazoshughulikiwa katika mtaala. • Tano, tafadhali fahamu kwamba wanafunzi hawapimwi kwenye kazi zao za usomaji. Haya yametolewa ili kuwasaidia wanafunzi kupata uelewa kamili wa kile moduli inafundisha, lakini haihitaji wanafunzi wako wawe wasomaji bora ili kuelewa kinachofundishwa. Kwa wale ambao mnapokea moduli hii katika tafsiri yoyote mbali na Kingereza, usomaji unaohitajika unaweza kuwa haupatikani katika lugha yako. Tafadhali chagua kitabu kimoja au viwili vinavyopatikana katika lugha yako - kimoja ambacho unadhani kinawakilisha vema kile kinachofundishwa katika sehemu hii – na uwape wanafunzi wako kama mbadala. • Mwisho kabisa, anza kufikiri kuhusu maswali muhimu na maeneo ya mafunzo ya huduma ambayo ungependa kuchunguza pamoja na wanafunzi kwa kuzingatia maudhui ambayo yanashughulikiwa.
Kabla ya Kozi Kuanza
Made with FlippingBook flipbook maker