Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
1 6 8 /
U O N G O F U & W I T O
Kabla ya kila somo, unapaswa kutazama mara nyingine tena maudhui ya mafundisho ambayo yanapatikana kwenye DVD kwa kipindi husika cha darasa, na kisha uunde kipengele cha Makutano na Uoanishaji kwa somo hili.
Kabla ya Kila Somo
Pitia upya Mwongozo wa Mkufunzi ili kuelewa malengo ya somo na kukusanya mawazo kwa ajili ya shughuli zinazowezekana za Makutano. (Maeneo mawili hadi matatu ya Makutano ambayo unaweza kutumia yametolewa, au jisikie huru kuunda yako, ikiwa hiyo inafaa zaidi.) Kisha, unda kipengele cha Makutano ambacho kinawatambulisha wanafunzi kwa maudhui ya somo na kukamata shauku zao. Kama sheria, mbinu za Makutano huweza kuwa katika makundi haya matatu kwa ujumla. Zinazochochea Umakini wa Kuzingatia hukamata umakini wa wanafunzi na kuwatambulisha kwenye mada ya somo. Vichocheo vya umakini wa kuzingatia vinaweza kutumika vyenyewe hasa kwa wanafunzi wenye hamasa au vikatumiwa kwa pamoja na moja wapo ya mbinu nyingine zinazoelezewa hapa chini. Mifano: • Kuimba wimbo wa ufunguzi unaohusiana na mada ya somo. • Kuonyesha kibonzo au mzaha unaohusiana na suala linaloshughulikiwa na somo. • Kuwaomba wanafunzi wasimame upande wa kushoto wa chumba ikiwa wanaamini kwamba ni rahisi kuwafundisha watu namna ya kuokolewa kutokea kwenye Injili, na kusimama upande wa kulia ikiwa wanaamini kuwa ni rahisi kuwafundisha watu kuokoka kutokea kwenye Nyaraka. Mbinu za Kusimulia hadithi aidha mwalimu aeleze hadithi inayoonyesha umuhimu wa maudhui ya somo au awaombe wanafunzi washiriki uzoefu wao (hadithi) kuhusiana na mada ambayo itajadiliwa. Mifano: • Katika somo la wajibu wa mchungaji, Mshauri anaweza kusimulia hadithi ya kuendesha mazishi na kushiriki maswali na changamoto ambazo zilikuwa sehemu ya uzoefu. • Katika somo kuhusu uinjilisti, Mshauri anaweza kuwaomba wanafunzi kueleza uzoefu ambao wamekuwa nao kuhusu kuhubiri Injili.
Kuandaa Kipengele cha Makutano
Made with FlippingBook flipbook maker