Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

/ 1 6 9

U O N G O F U & W I T O

Shughuli za kuibua maswali ibua maswali yenye changamoto kwa wanafunzi kujibu na kuwaongoza kuelekea maudhui ya somo kama chanzo cha kujibu maswali hayo, au yanaweza kuwataka wanafunzi waorodheshe maswali yao yaliyokosa majibu kuhusu mada itakayojadiliwa. Mifano: • Kuwasilisha mifano halisi inayotokea kwenye huduma ambayo inahitaji uamuzi wa kiuongozi na kuwafanya wanafunzi wajadili jibu ambalo lingekuwa bora zaidi. • Matatizo yaliyowekwa kwenye mfumo wa maswali kama vile, “Wakati wa kuhubiri kwenye mazishi, ni muhimu zaidi kwa mhudumu kuwa mkweli au mwenye huruma? Kwa nini? Bila kujali ni njia gani imechaguliwa, funguo ya kipengele cha Makutano iliyofaulu zaidi ni kutengeneza mpito kutoka kwenye Makutano hadi kwenye Maudhui ya Somo. Wakati wa kupanga kipengele cha Makutano, Washauri wanapaswa kuandika taarifa ya mpito ambayo hujenga daraja kutoka kwenye Makutano hadi kwenye Maudhui ya somo. Kwa mfano, ikiwa maudhui ya somo yalikuwa juu ya ukweli kwamba Roho Mtakatifu ni nafsi ya kiungu ambaye ni mshiriki kamili wa Uungu, shughuli ya Makutano inaweza kuwa ni kuwataka wanafunzi wachore haraka ishara inayomwakilisha vema zaidi Roho Mtakatifu kwao. Baada ya kuwafanya washiriki michoro yao na kujadili kwa nini walichagua walichofanya, Mshauri anaweza kutoa taarifa ya mpito kwa kufuata mistari ifuatayo: Kwa sababu Roho Mtakatifu mara nyingi huwakilishwa kwa ishara kama moto au mafuta katika Maandiko badala ya sura ya kibinadamu kama Baba au Mwana, wakati mwingine ni vigumu kuwasaidia watu kuelewa kwamba Roho Mtakatifu ni nafsi kamili ndani ya Uungu ambaye anafikiri, anatenda, na kuzungumza kibinafsi kama Uongofu & Wito, au Yesu Kristo. Katika somo hii, tunataka kuweka msingi wa kimaandiko wa kuelewa kwamba Roho ni zaidi ya ishara tu ya “nguvu za Mungu” na kufikiri njia ambazo tunaweza kulifanya hili kuwa wazi kwa watu katika makutaniko yetu. Hii ni kauli ya mpito yenye manufaa kwa sababu inaelekeza wanafunzi kwa kile wanachoweza kutarajia kutoka kwenye maudhui ya somo na pia inawatayarisha kwa baadhi ya mambo ambayo yanaweza kujadiliwa katika sehemu ya Uoanishaji itakayokuja baadaye. Ingawa unaweza kuifanya taarifa yako ya mpito kwa namna yako kulingana na majibu ya wanafunzi wakati wa kipengele cha Makutano, ni muhimu, wakati wa kupanga, kufikiri kitakachosemwa.

Made with FlippingBook flipbook maker