Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
1 7 0 /
U O N G O F U & W I T O
Maswali matatu yenye msaada katika kutathmini kipengele cha Makutano ulichokiunda ni: • Je, ni ya kibunifu na kufurahisha? • Je, inazingatia mahitaji na maslahi ya kundi husika? • Je, inawaelekeza watu kwenye maudhui ya somo na kuamsha shauku zao kwa maudhui hayo? Mara nyingine tena, pitia Mwongozo wa Mkufunzi ili kuelewa malengo ya somo na kukusanya mawazo kwa ajili ya shughuli zinazowezekana na Uoanishaji. Kisha, unda kipengele cha Uoanishaji ambacho huwasaidia wanafunzi kuunda uhusiano mpya kati ya ukweli na maisha yao (matokeo) na kujadili mabadiliko mahususi katika imani, mitazamo, au matendo yao ambayo yanafaa kutokea kama matokeo (matumizi). Unapopanga, kuwa mwangalifu kidogo na kosa la kufanya kipengele cha Uoanishaji kiwe wazi kupita kiasi. Kiujumla, sehemu hii ya somo inapaswa kuja kwa wanafunzi kama mwaliko wa kugundua, badala ya kama bidhaa iliyokamilika yenye matokeo yote mahususi yaliyoamuliwa mapema. Kwenye moyo wa kila kipengele kizuri cha Uoanishaji lipo swali (au mfululizo wa maswali) linalowauliza wanafunzi jinsi gani kujua ukweli kutakavyobadili mawazo, mitazamo, na tabia zao. (Tumejumuisha baadhi ya maswali ya Uoanishaji ili “kuwachochea” wanafunzi wako na mawazo yao, na kuwasaidia kuzalisha maswali yao wenyewe kutokana na uzoefu wao wa maisha.) Kwa sababu haya ni mafunzo ya kitheolojia na huduma, mabadiliko tunayohusika nayo zaidi ni yale yanayohusiana na namna ambayo wanafunzi wanajifunza na kuwaongoza wengine katika muktadha wa huduma. Jaribu na uzingatie katika kuwasaidia wanafunzi kufikiri kuhusu eneo hili la matumizi katika maswali unayoyatengeneza. Kipengele cha Uoanishaji kinaweza kutumia idadi ya miundo tofauti. Wanafunzi wanaweza kujadilimatokeonamatumizi pamoja katika kundi kubwa linaloongozwa na Mshauri au katika vikundi vidogo na wanafunzi wengine (ama majadiliano ya wazi au kufuata seti ya maswali yaliyoandikwa mapema). Mifano halisi, pia, mara nyingi ni vianzilishi vizuri vya majadiliano. Bila kujali mbinu, katika sehemu hii Mshauri na kikundi chenyewe cha kujifunza wanapaswa kuonekana kama chanzo
Kuandaa Kipegele cha Uoanishaji
Made with FlippingBook flipbook maker