Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
/ 1 7 1
U O N G O F U & W I T O
cha hekima. Kwa kuwa wanafunzi wako wenyewe tayari ni viongozi wa Kikristo, mara nyingi kuna utajiri wa uzoefu na maarifa ambayo yanaweza kutoka kwa wanafunzi wenyewe. Wanafunzi wanapaswa kutiwa moyo kujifunza kutoka kwa kila mmoja wao na vile vile kutoka kwa Mshauri. Kanuni kadhaa zinapaswa kuongoza mijadala ya Uoanishaji unayoongoza: • Kwanza, lengo la msingi la kipengele hiki ni kuyaibua maswali waliyonayo wanafunzi. Kwa maneno mengine, maswali yanayotokea kwa wanafunzi wakati wa somo huchukua kipaumbele juu ya maswali yoyote ambayo Mshauri hutuyarisha mapema- ingawa maswali yanayoulizwa na Mshauri mzoefu bado yatakuwa zana muhimu ya kujifunzia. Sambamba na hili ni kukisia kwamba swali liloibuliwa na mwanafunzi mmoja mara nyingi huwa ni swali lisilozungumzwa lililopo kwa kundi zima. • Pili, jaribu na uelekeze mjadala kwenye hali halisi na maalum badala ya nadharia au hali dhahania tu. Sehemu hii ya somo inakusudiwa kuzingatia hali halisi ambazo wanafunzi mahususi darasani wanakabiliana nazo. • Tatu, usiogope kushiriki hekima ambayo umepata kupitia uzoefu wako mwenyewe wa huduma. Wewe ni nyenzo muhimu kwa wanafunzi na wanapaswa kutarajia kwamba utafanya masomo uliyowahi kujifunza yapatikane kwa ajili yao. Hata hivyo, kumbuka kila wakati kwamba vigezo vya kitamaduni, muktadha, na haiba vinaweza kumaanisha kwamba kilichofanya kazi kwako kinaweza kisifanye kazi kwa kila mtu kila wakati. Toa mapendekezo, lakini zungumza na wanafunzi kuhusu kama uzoefu wako unaonekana kutekelezwa katika muktadha wao, na kama sivyo, ni marekebisho gani yanaweza kufanywa ili kufanya hivyo. Maswali Matatu muhimu ya kutathmini kipengele cha Uoanishaji ulichounda ni: • Je, nimetazamia mapema ni maeneo yapi ya jumla ya matokeo na matumizi yanayoweza kuwepo kwenye mafundisho yanayotolewa kwenye somo? • Je, nimeunda njia ya kuibua maswali ya wanafunzi na kuyapa kipaumbele? • Je, hii itamsaidia mwanafunzi kuondoka darasani akijua la kufanya na ukweli aliojifunza?
Made with FlippingBook flipbook maker