Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
1 7 2 /
U O N G O F U & W I T O
Hatimaye, kwa sababu Project ya huduma ni kazi yamatumizi ya ukweli iliyopangwa kwa kozi nzima, itakuwa muhimu kutenga sehemu ya kipengele cha Uoanishaji ili wanafunzi wajadili kile wanachoweza kuchagua kwa kazi yao na kutathmini maendeleo na/au kuripoti kwa darasa kufuatia kukamilika kwa kazi hiyo.
Hatua za Kuongoza Somo • Chukua mahudhurio. • Ongoza ibada. • Sema au imba Ukiri wa Nikea na uombe • Simamia jaribio
Shughuli za Ufunguzi
• Angalia kazi ya kukariri Maandiko • Kusanya kazi zozote zinazotarajiwa.
• Tumia Makutano yaliyotolewa katika Mwongozo wa Mkufunzi, au uunde yako.
Fundisha Kipengele cha Makutano
• Wasilisha Maudhui ya somo kwa kutumia mafundisho ya video. Kutumia Sehemu za Video
Simamia Kipengele cha Maudhui
Kila somo lina sehemu mbili za mafundisho ya video, kila moja ikiwa na urefu wa takribani dakika 25. Baada ya kufundisha kipengele cha Makutano (ikiwa ni pamoja na taarifa ya mpito), cheza sehemu ya kwanza ya video kwa ajili ya wanafunzi. Wanafunzi wanaweza kufuatilia wasilisho hili kwa kutumia Kitabu chao cha Kazi ambacho kina muhtasari wa jumla wa nyenzo zinazowasilishwa na marejeo ya Maandiko na nyenzo za ziada zinazorejelewa na mzungumzaji. Mara baada ya sehemu ya kwanza kutazamwa, shirikiana na wanafunzi ili kuthibitisha kuwa maudhui yalieleweka.
Made with FlippingBook flipbook maker