Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

/ 1 7 7

U O N G O F U & W I T O

Neno Linaloumba

MAELEZO YA MKUFUNZI 1

Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi, Somo la 1, Neno linaloumba. Lengo la jumla la moduli ya Uongofu na Wito ni kuwawezesha watenda kazi na viongozi wa Kikristo wa mijini kuthamini, kuthibitisha, na kutumia Maandiko katika kila nyanja ya maisha na huduma zao. Zaidi ya vyanzo vingine vyote, nyenzo, na vifaa ambavyo mwanamume au mwanamke wa Mungu anaweza kutumia ili kumwakilisha Kristo na Ufalme wake, hakuna jambo la maana zaidi kuliko Neno la Mungu kama kipimo kikuu na cha mwisho cha ukweli na utendaji kwa ajili ya uanafunzi wa Kikristo. Kazi yako katika somo hili ni kuwasaidia wanafunzi wako kugundua nguvu ya Maandiko, hasa katika jukumu lake la kumbadilisha Mkristo na kuthibitisha wito wa Mungu katika maisha ya kiongozi. Zingatia kwamba kila somo limeeleza malengo ya kujifunza, na malengo haya yanakusudiwa kutumika kama miongozo kwako katika somo zima; yameelezwa kwa uwazi, na unapaswa kuyasisitiza katika somo lote, na kuyarejelea hasa wakati wa majadiliano na wanafunzi. Kadiri unavyoweza kuangazia malengo katika kipindi chote cha darasa, ndivyo utakavyotoa nafasi nzuri zaidi kwa wanafunzi kuweza kuelewa na kufahamu ukubwa wa malengo haya. Katika somo hili, utazingatia asili ya Neno la Mungu kuumba maisha mapya. Zingatia kipengele hiki cha uwezo wa kiuumbaji katika uongozi wako wa somo. Kwa mara nyingine tena, hakikisha kwamba unatayarisha kipindi chako cha darasa kimahususi kwa kuzingatia malengo haya, na usisite kuwashirikisha wanafunzi juu ya malengo haya kwa ufupi darasani kabla ya kuanza kipindi. Vuta usikivu wa wanafunzi kuelekea malengo haya, kwani, kiuhalisia, huu ndio moyo wa dhumuni lako la kielimu unapofundisha vipindi vya somo hili. Kila kitu kinachojadiliwa na kufanyika kinapaswa kulenga kwenye malengo haya. Tafuta njia za kuyasisitiza haya kila wakati, kuyakazia na kuyarudia tena na tena unapoendelea na somo Pengine mojawapo ya masuala magumu sana utakayopaswa kukabiliana nayo kwa wanafunzi wako ni mwelekeo wa kulichukulia Neno la Mungu kirahisi. Wale wanaohudumia wengine wana mwelekeo wa kupuuza raha na nguvu ya Neno la Mungu kwa ajili ya maisha yao wenyewe; katika haraka yao ya kuhudumu na kufanya kazi pamoja na wengine na kwa ajili ya wengine, wanaweza kujikuta wamekauka na kuishiwa, bila lishe na nuru ya kiroho ifaayo. Ibada hii inalenga katika hazina ya

 1 Ukurasa 15 Utangulizi wa Somo

 2 Ukurasa 15 Malengo ya Somo

 3 Ukurasa 15 Ibada

Made with FlippingBook flipbook maker