Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
1 7 8 /
U O N G O F U & W I T O
ajabu ambayo ni Neno la Mungu, na inatupa changamoto ya kulizingatia kwanza kama chakula chetu wenyewe na chanzo cha maisha yetu, kisha kama silaha ya lazima katika huduma. Katika nyanja zote za maisha na huduma, hakuna kitu kinachotoa nguvu, kutia moyo, na kuleta burudiko kama Neno la Mungu.
Sala hizi hazipaswi kuonekana kuwa sehemu tu ya somo bali kama kiashiria cha kihistoria na cha kiroho cha shauku tuliyo nayo kwamba Mungu atuwezeshe kulijua na kulitumia Neno lake. Ni Mungu pekee kupitia Roho wake anayeweza kutuwezesha kuona na kuthaminiNeno lake takatifu ipasavyo.Wahimizewanafunzi kumtegemea Bwana ili kuwasaidia kuelewa nguvu ya Neno Linaloumba. Mifano hii ya kipengele hiki hutafuta kutengeneza muktadha ambao wanafunzi wanaweza kuanza kupata picha ya mawasilisho yanayofuata. Mifano hii imekusudiwa kuwasaidia wanafunzi kutafakari juu ya nafasi ya Neno la Mungu katika hali mbalimbali, umuhimu wake, na jukumu lake katika kushughulikia masuala na kutatua matatizo. Tumia mifano hii kuwasaidia wanafunzi kujadili kuhusu nafasi ya Maandiko katika miktadha mbalimbali yenye maana katika jamii na katika maisha yao. Mojawapo ya malengo makuu ya somo hili ni kuwasaidia wanafunzi kukua katika staha, heshima, na kicho kwa habari ya Neno la Mungu. Neno la Mungu ni la uumbaji na bora sana, kiasi kwamba kiongozi wa Kikristo wa mjini lazima ajifunze kuyapenda Maandiko kama chakula chake mwenyewe, na kuyathamini sana kwa sababu ya ubora na sifa zake za asili. Hakuna lugha bora zaidi ya kuelezea nguvu na hekima iliyomo katika Neno la Mungu; usihofu kukazia ubora wa Maandiko, na kuwapa changamoto wanafunzi kupenda na kutumia Maandiko kama hazina inayotambulika kuwa ni Neno la Mungu mwenyewe.
4 Ukurasa 16
Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi
5 Ukurasa 17 Kujenga Daraja
6 Ukurasa 21 Muhtasari wa Kipengele I-C-5
Ukweli uliopo hapa ni kuhusu jukumu la Neno la Mungu kama nyenzo ambayo Mungu wa Utatu alitumia kuumba ulimwengu. Kile ambacho ni kweli kuhusu nyenzo inayotumiwa na Mungu katika mambo ya uumbaji-asilia pia ni kweli katika
7 Ukurasa 22 Muhtasari wa Kipengele II-C-3
Made with FlippingBook flipbook maker