Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

/ 1 7 9

U O N G O F U & W I T O

ulimwengu wa roho, yaani, jambo ambalo Mungu anaamuru kupitia nguvu za Neno lake linatimizwa. Inatokea, si tu kipindi cha mwanzo (Mwa. 1; Zab. 33:6,9; 148:5), bali pia ni kweli kuhusu utendaji wa Mungu katika ulimwengu wa asili (Zab. 105:31,34; 104:7; 147:18) na pia katika historia yote (Zab. 107:20; taz. Hekima ya Sira 16:12). Angalia hapa katika simulizi hizi mbalimbali kwamba kusema na kutenda kwa Mungu kunatofautishwa nyakati fulani katika Maandiko (kama vile pia katika Isa. 45:12; 48:13), lakini utendaji wa uumbaji wa Mungu haupaswi kueleweka tu katika mambo anayosema (taz. pia Eze. 37:4-6; Isa 48:3). Roho Mtakatifu wa Mungu anahusika kwa ukaribu katika Neno lake na kazi yake, kama inavyoonekana katika Mwa. 1:2 na Isa. 34:16; Ayubu 37:12. Maswali haya yameundwa ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa malengo muhimu na ukweli unaowasilishwa katika sehemu hii ya kwanza ya video. Utalazimika kugawa muda wako vizuri, haswa ikiwa wanafunzi wako wamevutiwa na dhana hizi, na wanataka kujadili maana zake kwa urefu. Ruhusu muda ufaao wa kuangazia mambo makuu, na bado uwe na muda wa kutosha wa mapumziko kabla ya sehemu inayofuata ya video kuanza. Tena, zingatia hasa malengo ya sehemu ya kwanza, na utumie maswali haya kukazia na kufafanua kwa undani kweli zinaohusiana na uwasilishaji uliotangulia. Pia, tumia muda wa maswali na majibu kuwekea mkazo mada na masuala yanayowavutia wanafunzi wako, au mawazo unayoamini ni muhimu hasa kulingana na namna unavyowafahamu wanafunzi wako. Nguvu ya uumbaji ya Neno la Mungu inaonekana kimwili na kiroho katika somo hili, na mjadala wako unapaswa kuangazia kipengele hiki chenye nguvu cha Maandiko. Ukweli kwamba Neno la Mungu lina nguvu maalum katika uumbaji wa Mungu labda umeelezwa kwa muhtasari bora zaidi katika Zaburi 147:15-20: Huipeleka amri yake juu ya nchi, Neno lake lapiga mbio sana. 16 Ndiye atoaye theluji kama sufu, Huimwaga barafu yake kama majivu, 17 Hutupa mvua ya mawe kama makombo, Mbele ya baridi yake ni nani awezaye kusimama? 18 Hulituma neno lake na kuviyeyusha, Huuvumisha upepo wake, maji yakatiririka. 19 Humhubiri Yakobo neno lake, Na Israeli amri zake na hukumu zake. 20 Hakulitendea taifa lo lote mambo kama hayo, Wala hukumu zake hawakuzijua. Haleluya.

 8 Ukurasa 25 Maswali kwa Wanafunzi na Majibu

 9 Ukurasa 34 Maswali kwa Wanafunzi na Majibu

Made with FlippingBook flipbook maker