Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

1 8 0 /

U O N G O F U & W I T O

Andiko hili linaangazia kanuni ambayo inafaa kujadiliwa kwa kina na kueleweka katika kipindi hiki cha maswali na majibu.

Katika sehemu hii zilizoorodheshwa ni kweli za kimsingi zilizoandikwa katika mfumo wa sentesi ambazo wanafunzi wanatakiwa kuwa wamezipokea kutoka kwenye somo hili, yaani kutoka kwenye video walizotazama na mijadala waliyoifanya chini ya uongozi wako. Usisite kurudia dhana au kweli hizi kwa msisitizo. Hakikisha kwamba dhana hizi zimefafanuliwa vizuri na zimewekewa mkazo kwa umakini mkubwa, kwasababu, maswali ya majaribio na ya mtihani wa mwisho yatatokana moja kwa moja na dhana hizo. Muhimu zaidi, tafuta kutumia muda vizuri ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa mawazo haya ya msingi ambayo yanafafanua somo hili. Katika kuwasaidia wanafunzi wako kufikiria hali zao wenyewe, unaweza kubuni baadhi ya maswali au kutumia yale yaliyotolewa hapa chini kama tu njia ya kuchochea shauku yao. Kilicho muhimu hapa sio maswali yaliyoandikwa hapa chini, lakini ni kwako wewe, katika mazungumzo na wanafunzi wako, kutatua kada ya masuala kadha wa kadha, mashaka, maswali, na mawazo ambayo yanatokana moja kwa moja na uzoefu wao, kisha husianisha hayo na maisha na huduma zao. Usisite kutumia muda mwingi kwa ajili swali fulani lililotokana na video, au jambo maalum ambalo linafaa hasa katika muktadha wa huduma wanazofanya wakati huu. Lengo la sehemu hii ni kuwawezesha kufikiri kwa kina na kitheolojia kuhusiana na maisha yao na mazingira ya huduma zao. Kwa mara nyingine, maswali yaliyo hapa chini yametolewa kama miongozo na vichocheo tu, na hayapaswi kuonekana kama ya lazima. Chagua na uchukue kutoka katika hayo, au utengeneze maswali yako mwenyewe. Jambo la muhimu ni tija ya maswali hayo sasa, kwa muktadha wao na kwa maswali yao.

 10 Ukurasa 35 Muhtasari wa Dhana Muhimu

 11 Ukurasa 36 Kutendea Kazi Somo na Matokeo Yake kwa Mwanafunzi

Kusudi la kipengele hiki cha mifano halisi ni kuwaruhusu wanafunzi kutumia kwa ubunifu katika mazingira halisi au ya kufikirika kweli ambazo wamekuwa wakizijadili darasani. Kitaalam hakuna majibu sahihi kwa maswali ya eneo hili kwa maana ya njia moja tu inayoweza kutumika kuyashughulikia au kuyaelewa.

 12 Ukurasa 36 Mifano Halisi

Made with FlippingBook flipbook maker