Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

/ 1 8 1

U O N G O F U & W I T O

Unachotafuta kupitia uzingatiaji wako wa masuala haya ni uwezo wa wanafunzi kuunganisha masomo yao na hali halisi za huduma ambazo zitadai utambuzi wao, tiba, na upembuzi makini wa masuala na matatizo ya kiroho. Kwa maana halisi, mifano halisi inahusu utatuzi bunifu wa matatizo, kwa hivyo wasaidie wanafunzi kutafuta kuunganisha elimu yao na masuala makuu yanayohusishwa na hali husika. Watake wanafunzi waainishe masuala yanayohitaji kusuluhishwa, na waeleze kanuni za kibiblia zinazohusiana na maoni yao. Wasaidie kueleza misimamo yao kwa uwazi, na uhimize mjadala baina ya wanafunzi kuhusu kweli wanazojifunza. Kila somo linatoa nafasi kwa kila mwanafunzi kuzingatia jinsi kweli mahususi za somo husika zinavyohusiana na maisha na huduma zao mahususi. Bila shaka, kanuni unazoshughulikia zinahusiana na maisha ya wanafunzi, na ikiwa unajua jinsi gani, unaweza kuzisisitiza, au kuwasaidia wanafunzi kuona miunganiko, na kuitikia ipasavyo kama wanaweza. Matumizi ya Neno la Mungu katika maisha yao binafsi ndilo lengo la sehemu hii. Wahimize wanafunzi kutafakari maisha yao binafsi ili kuona jinsi Roho Mtakatifu anaweza kuwataka kutumia kweli hizi katika maisha yao wiki hii. Kuwa tayari, ikiwa muda unaruhusu, kwa uhitaji wa ushauri na maombi mahususi ambao wanafunzi wako wanaweza kuwa nao katika maisha na huduma zao. Lengo la elimu yoyote ya kitheolojia na misiolojia ni kuwawezesha wanafunzi kibinafsi kufanya Neno la Mungu kuwa hai katika maisha yao binafsi na kupitia kwao katika makusanyiko yao na huduma zinazobubujika kutoka ndani yao. Namna unavyowafahamu wanafunzi wako kibinafsi, na uwazi wao kwako unapaswa kutoa fursa ya kiwango fulani cha ushauri wako kwao. Usilazimishe hilo kwa wanafunzi wako, lakini uwe wazi pale litakapohitajika, na ulitarajie. Maandiko yatawaweka wazi wanafunzi wako kwa Mungu na mpango wake, kwa hivyo utayari wako wa kuwasaidia kimahususi na kwa uthabiti ni sehemu muhimu ya jukumu lako la ushauri kwao. Wakumbushe wanafunzi kwamba Neno la Mungu ni kwa ajili ya matumizi, sio tu kutafakari na majadiliano (Yakobo 1:22-25). Acha Roho Mtakatifu akuongoze unapowasikiliza na kuwajibu wanafunzi wako.

 13 Ukurasa 39 Kuhusianisha Somo na Huduma

 14 Ukurasa 39 Ushauri na Maombi

Made with FlippingBook flipbook maker