Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

1 8 2 /

U O N G O F U & W I T O

Usimamiaji wa maekelezo ya kozi, pamoja na kutunza kumbukumbu na kudumisha mawasiliano mazuri, ni sehemu kuu ya jukumu lako kama mkufunzi. Pamoja na hayo, ni muhimu uhakikishe kwamba wanafunzi wanaelewa zoezi la wiki ijayo, hasa lile la uandishi. Hili sio gumu; lengo ni kwamba wasome maudhui vizuri wawezavyo na kuandika sentensi chache juu ya kile ambacho waandishi walimaanisha. Huu ni ujuzi wa kiakili muhimu kwa wanafunzi wako kujifunza, kwa hivyo hakikisha kwamba unawatia moyo katika mchakato huu. Bila shaka, kwa wale wanafunzi ambao uwezo wao unafanya zoezi hili kuwa mzigo na/au gumu, wahakikishie kwamba nia ya kazi hii ni kuwahimiza kuelewa maudhui ya somo, na si kuonyesha ujuzi wao wa kuandika. Ingawa uboreshaji wa ujuzi wa kuandika ni lengo linalofaa, hatutaki kusisitiza ujuzi kama huo kwa namna itakayoathiri vibaya lengo la kuwatia moyo na kuwajenga. Wala, hata hivyo, hatutaki kudunisha uwezo wao. Tafuta namna bora itakayofanikisha malengo yote mawili: kuwapa changamoto na kuwatia moyo.

 15 Ukurasa 39 Kazi

Made with FlippingBook flipbook maker