Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
/ 1 8 3
U O N G O F U & W I T O
Neno Linalothibitisha
MAELEZO YA MKUFUNZI 2
Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi, Somo la 2, Neno linalothibitisha . Lengo la jumla la somo hili katika moduli hii ya Uongofu na Wito ni kuangazia na kusisitiza uwezo wa Neno la Mungu wa kuthibitisha, si tu kwa habari ya dhambi ya mtu mbele za Mungu bali pia ukweli wa ushuhuda wake kuhusu Kristo na Ufalme wake. Uwezo huo umeunganishwa moja kwa moja na nguvu ya Neno ya kugeuza, iliyozingatiwa katika somo letu lililopita, na bado unasisitiza uhusiano wa Biblia na ukweli na uhalisia. Kweli hizi ni muhimu kwa kiongozi wa mjini kuelewa, kueleza na kutumia. Angalia tena jinsi malengo husika yalivyoelezwa kwa uwazi. Kama kawaida, jukumu lako kama Mkufunzi ni kusisitiza dhana hizi wakati wote wa somo, hasa wakati wa majadiliano na wanafunzi. Kadiri unavyoweza kuangazia malengo katika kipindi chote cha darasa, ndivyo uwezekano unavyokuwa mkubwa zaidi wa wao kuelewa na kufahamu ukubwa wa malengo haya. Kuthibitisha [kwa maana ya kuhukumiwa moyoni] kwa kawaida hueleweka katika maana ya huzuni, kama kitu ambacho mtu hukipitia baada ya kutambua kosa, ama dhidi ya Mungu au dhidi ya wengine. Ibada hii inadokeza kwamba kuthibitishiwa kwa hakika ni aina ya pekee ya hali ambayo inaweza kuleta hisia ya huzuni, lakini hisia hiyo ya huzuni inaongoza kwenye uponyaji, nuru, na mabadiliko. Kuthibitisha ni kazi ya Bwana; hakuna mtu ambaye kwa nguvu zake mwenyewe anaweza kutoa uthibitisho. Hata hivyo, twaweza kuwa wazi sana kwa Mungu kiasi cha kumruhusu atuelekeze na kutufundisha, atuhakikishie kuhusu uhalisia wa hali yetu, kuhusu uhalisia wa nia yake, na mpango wake kwa ajili ya maisha yetu ni nini. Kutokuwa na uwezo wa kushawishika ni mahali pa kutisha kuwepo; mtu anapofika mahala pa kumwelewa Mungu ni nani na nia yake ni nini, basi hapo ndipo tu anapoweza kugundua nafasi yake halisi katika mpango wake – utambulisho wetu jinsi ulivyo, na sio tu kama tunavyojifikiria. Sala ya Luther inaangazia fundisho kuu la somo hili, ambalo ni uwezo wa Baba kutuwezesha kuchukua vipawa vyake na kweli zake kwa njia ya Roho Mtakatifu katika jina la Yesu Kristo. Mungu hutuwezesha kuona ukweli wake, kuona mambo jinsi yalivyo, na kupitia kuona huko, tunatiwa nguvu za kutumiwa na Mungu kwa njia za ajabu. Uwezo huu wa kuona hautokei hivi hivi wala hauko kwa kila mtu ilimradi. Uwezo wetu wa kuona unahusiana moja kwa moja na uwezo wetu wa
1 Ukurasa 43 Utangulizi wa Somo
2 Ukurasa 44 Ibada
3 Ukurasa 44
Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi
Made with FlippingBook flipbook maker