Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

1 8 4 /

U O N G O F U & W I T O

kujifunza, kufundishwa na Bwana, kusadikishwa na Neno lake na utendaji wake ulimwenguni. Siku zote maombi yetu ya kina sana lazima yawe kwamba Mungu atuhakikishie kwa habari ya kweli ili tuweze kutumiwa naye katika njia zinazofaa.

Jaribio linahusu baadhi ya mawazo na masuala makuu yaliyoangaziwa wiki iliyopita. Tumia jaribio kama mbinu ya kufanya marudio ya kweli zilizofundishwa kupitia mawasilisho yako na mijadala mbalimbali darasani wiki iliyopita; usijali sana kuhusu alama na ufaulu; majaribio na mitihani katika moduli hii imewekwa kimakusudi kwa matumizi yako kama zana za kufundishia – mbinu za kuwakumbusha wanafunzi kuhusu masuala muhimu ya moduli. Ikiwa muda unaruhusu, unaweza kufanya masahihisho ya jaribio na kujadili majibu sahihi darasani. Hata hivyo, katika somo hili na mengine yote suala la ufinyu wa muda ni halisi sana, kwa hiyo uwezekano mkubwa ni kwamba utaamua kutoa jaribio na kisha kusahihisha baadaye. Ni muhimu sana kusisitiza jukumu la kukariri Maandiko – fanya hivyo kwa nguvu zote na kwa makusudi. Wakumbushe wanafunzi kuhusu nafasi ya zoezi hili katika ufaulu wao, na pia (na muhimu zaidi) umuhimu wake katika jukumu lao la uongozi. Maandiko yaliyofichwa moyoni yanapatikana mara moja kwa ajili ya matumizi na ushauri, pamoja na kuwa nyenzo iliyo tayari kwa ajili ya kutaamuli na kutafakari. Hii ni nidhamu na itadai kwamba wanafunzi wafanyie kazi mistari husika mara kwa mara na kwa uaminifu katika wiki nzima, na sio tu kama kazi ya kipindi cha darasa. Kama nyenzo inayotumiwa na Mungu kuleta uthibitisho ndani ya moyo, Neno la Mungu linaweza kutumiwa vibaya kwa urahisi kwa sababu tu ya nia njema ya kushughulikia masuala ya kimaadili na kinidhamui. Mara nyingi uthibitisho ambao Mungu huleta ndani ya mtu umekusudiwa kuleta uhuru na shangwe maishani mwetu, si kutufanya tuwe watumwa wa viwango vya maadili vya mtu huyu au mtu yule au kikundi fulani cha watu. Moja ya ujuzi muhimu kwa kiongozi wa Kikristo kujifunza, ni wakati gani na wapi Neno la Mungu linatumiwa kwa usahihi ili kuwaleta watu kwenye huzuni ya kimungu iletayo toba ya kweli, au pale ambapo linatumiwa kama kigezo cha kujenga utumwa na hukumu zisizo za kimungu kati ya

 4 Ukurasa 45 Jaribio

 5 Ukurasa 45 Mazoezi ya Kukariri Maandiko

 6 Ukurasa 45 Kujenga Daraja

Made with FlippingBook flipbook maker