Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
/ 1 8 5
U O N G O F U & W I T O
waamini. Neno la Mungu linadai ufahamu wenye hekima na uerevu, na mifano ya kipengele hiki imekusudiwa kuwafanya wanafunzi waangalie jinsi Neno la Mungu linavyotumika kutambua kile ambacho ni cha dhambi, chema, kizuri n.k, iwe katika jamii au Kanisa. Angalia kwa makini asili ya mizozo katika mifano iliyotolewa hapa, na uweke mkazo katika kuwasaidia wanafunzi kuona jinsi Neno la Mungu linavyotumiwa kuleta uthibitisho na kufunua uhalisia wa ndani wa maisha ya watu. Tazama namna ambavyo kauli ya Yesu katika Yohana 16:7-11 inalenga katika huduma ya RohoMtakatifu ya kuthibitisha, na hoja ya somo hili ni kwamba nyenzo yake kuu anayotumia kuthibitisha ni Neno la Mungu. Ni muhimu katika kufikiria kazi ya Roho Mtakatifu kwamba wanafunzi waone uwiano kati ya Neno la Mungu na huduma ya Roho, hasa ile ya kuthibitishia watu kwa habari ya dhambi, haki, na hukumu. Si vyema kamwe kutenganisha nguvu ya Neno la Mungu na utendaji, uvuvio, na uongozi wa Roho Mtakatifu, au kinyume chake; Maandiko ni Neno la Roho pekee, kwa kuwa yeye ndiye mwandishi wake kupitia uongozi na uvuvio wake (2 Pet. 1:19-21). Katika kuzungumza juu ya uwezo wa Maandiko wa kuthibitisha kuhusu dhambi kupitia utendaji kazi wa Roho Mtakatifu, ni muhimu kwamba tusisitize pamoja na wanafunzi wazo la uhusiano wa karibu kati ya Maandiko na utakatifu. Kwa asili yake, Neno la Mungu ni takatifu, kwa kuwa lilivuviwa na Mungu mtakatifu, na kuzalishwa kupitia huduma ya Roho Mtakatifu. Hili lina maana kubwa kwa wale wanaotamani kufanya wanafunzi mijini, ambako vitongoji vingi vinalemewa na athari za utovu wa maadili. Uwezo huu wa Neno la Mungu kuzalisha utakatifu ni sababu muhimu kwa nini tunapaswa kusisitiza mafundisho na mahubiri ya kibiblia katika kila hatua ya upandaji kanisa na maendeleo ya uongozi mijini. Waebrania 5:11-6:2 inakazia uwezo huo, kwa kuwa mwanamume au mwanamke wa Mungu aliyekomaa kupitia mazoezi ya kudumu ufahamu wake wa rohoni umezoezwa kupambanua lililo jema na baya. Hakuna lugha nzuri na nzito vya kutosha kusisitiza juu ya uwezo huu wa Neno la Mungu kwa wale wanaotamani kuona maisha yaliyobadilishwa katika kufanya wanafunzi mijini. Lengo lazima liwe kusisitiza juu ya uwezo wa Neno kufafanua mapenzi ya Mungu kwa uwazi na uhalisia wa hali yetu ya “kukosa shabaha” kuhusiana na mapenzi hayo.
7 Ukurasa 48 Muhtasari wa Kipengele I
8 Ukurasa 50 Muhtasari wa Kipengele I-C-3
Made with FlippingBook flipbook maker