Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

1 8 6 /

U O N G O F U & W I T O

Haki inafafanuliwa sio tu kwa lugha ya kimaadili katika Maandiko, bali pia katika suala la uhusiano wetu na Mungu kwa njia ya imani. Tofauti hii lazima ieleweke kwa uangalifu, kwa kuwa kama vile Maandiko hapo juu yanavyodokeza, haki haiangaziwi tu katika suala la mwenendo wetu wa haki au wa kiadili, bali pia katika suala la hadhi tuliyo nayo mbele za Mungu kwa sababu ya uhusiano wetu na Mungu kupitia Yesu Kristo. Uhusiano wetu na Mungu kwa imani katika Yesu Kristo umetufanya kuwa wenye haki machoni pa Mungu, na kwa sababu hiyo tunapaswa kujitahidi kuishi kwa haki mbele za Mungu katika tabia na mienendo yetu kwa kuwa tumehesabiwa haki machoni pake kwa sababu ya imani. Haki yetu tunayoiishi kila siku hutiririka kutokana na haki tuliyohesabiwa (tuliyopewa) ambayo tulipokea kutoka kwa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo. Tumia muda huu wa maswali na majibu kuangazia mawazomuhimu yanayohusiana na dhambi, haki, na hukumu. Ingawa maswali haya yanalenga katika kukuza uelewa wa maarifa na kweli zinazohusishwa na madai yaliyotolewa katika sehemu ya kwanza ya video, yatumie kama njia ya kuangazia na kuchanganua mada muhimu zilizojitokeza katika sehemu hiyo. Kwa maana hii, unatakiwa kutumia maswali haya kama zana ya uhakiki na pia zana ya kuibua mawazo na kuyafafanua. Zingatia kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa majibu yanayotolewa kulingana na malengo ya sehemu ya kwanza ya somo. Pia zingatia kutunza muda ili uweze kushughulikia maswali yaliyo hapa chini na yale yanayoulizwa na wanafunzi wako, na uwe makini na jambo lolote linaloweza kukutoa nje ya lengo la kufanya marudio ya kweli muhimu na mambo makuu ya sehemu hii ya somo. Kupitia mada ya uthibitisho, somo hili linaangazia mada muhimu katika Maandiko. Elimu kuhusu Yesu Kristo, asili na upeo wa Ufalme wa Mungu, na jukumu kuu la mitume na manabii, yote haya yanaenda moja kwa moja kwenye shina la ujumbe wa Biblia, na kwa pamoja yanawakilisha kiini kizima cha Maandiko yote. Uwezo wa Roho Mtakatifu wa kututhibitishia kwa habari ya Yesu, Ufalme, na Injili na ujumbe wa mitume ndio kiini cha imani yetu, na msingi wa kile tunachoita kuwa mahiri katika ujuzi wa Maandiko. Kwa uwazi, hakuna mtu anayeweza kudai kuwa na ustadi wa Maandiko ikiwa atapuuza au kuelewa vibaya elimu juu ya Kristo, nguvu za Ufalme, na nguvu ifunguayo ya mafundisho na Injili ya mitume. Hizi sio

 9 Ukurasa 51 Muhtasari wa Kipengele II-B-2

 10 Ukurasa 54 Maswali kwa Wanafunzi na Majibu

 11 Ukurasa 56 Muhtasari wa Kipengele I

Made with FlippingBook flipbook maker