Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

/ 1 8 7

U O N G O F U & W I T O

mada tu kati ya zingine, bali zinawakilisha mada na jumbe kuu za Agano la Kale na Agano Jipya.

Makazo huu juu ya uwezo wa Roho Mtakatifu wa kutuzoeza na kutufundisha kuhusu Ufalme na namna Yesu alivyouzindua hapa duniani kupitia maisha yake ni muhimu ili kuelewa nguvu ya uthibitisho ya Neno la Mungu. Vipaumbele vya Mungu katika kuthibitisha ni muhimu katika kuelewa mawazo na nia ya Mungu; lengo la moyo wa Mungu ni kutufundisha kuhusu mpango wake mkuu wa kuurudisha ulimwengu mzima chini ya mamlaka na kweli yake kuu. Kwa kuuingiza Ufalme duniani kupitia umwilisho wa Yesu Kristo, Mungu ameweka wazi kwamba ahadi alizotoa kwa Abrahamu sasa zimetimizwa kwa njia ya Yesu, na kwamba utawala wake, uliongojewa kwa muda mrefu, sasa kwa maana fulani kwa kweli umekuja, ingawa si katika utimilifu wake wala katika muundo wake wa mwisho. Roho anapozungumza, anakusudia kutusadikisha juu ya ukweli wa jambo hili tukufu, ambalo ni la msingi katika kujenga uelewa wa kazi ya Mungu ulimwenguni leo kupitia watu wake, Kanisa. Kanuni hii inasisitiza asili ya makusudi ya kinabii na kitume ya Neno la Mungu. Maandiko hutokeza uthibitisho, si tu kwa sababu ya ujumbe wake, bali pia kutokana na mchakato wake. Wale ambao Mungu Roho Mtakatifu aliwaongoza kuandika Maandiko waliteuliwa na kutiwa mafuta ili kumwakilisha kwa mamlaka ambayo ni ya mwisho na yasiyoweza kubatilishwa. Hakuna anayeweza kukataa kwamba wajumbe hawa na maandiko yao ni vyombo vya mwisho na visivyoweza kukanushwa ambavyo Mungu anavitumia kuzungumza, na kututhibitishia kwa habari ya ukweli wa nafsi yake na mapenzi yake. Ni muhimu kuangazia mada kuu za Maandiko hapa kwa kuzingatia umuhimu wake. Kwa maneno mengine, katika mazungumzo yako, usisite kusisitiza dhana muhimu kuhusu Kristo na Ufalme wake, na wajumbe wa kinabii na kitume katika jukumu lao kama wasemaji wa Neno la Mungu. Jadili masuala hayo kwa uwazi, hasa namna mada hizi tatu zinavyowakilisha kiini cha Neno la Mungu, na kwa namna hiyo zinapewa kipaumbele fulani katika kututhibitishia kwa habari ya kweli.

 12 Ukurasa 58 Muhtasari wa Kipengele II

 13 Ukurasa 60 Muhtasari wa Kipengele III

 14 Ukurasa 62 Maswali kwa Wanafunzi na Majibu

Made with FlippingBook flipbook maker