Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
1 8 8 /
U O N G O F U & W I T O
Wekea mkazo kwa uwazi dhana hizi, ukijadili kwa makini mada yoyote ambayo inawezakuwa haijaeleweka kikamilifu au bado unahitaji kuitolea ufafanuzi kwa namna endelevu kwa kuzingatia mijadala iliyopita.
15 Ukurasa 63 Muhtasari wa Dhana Muhimu
Wahimize wanafunzi wako kuuliza maswali, na usiwachukulie kama waliokengeushwa au waliojaa mashaka. Kwa kuuliza maswali waliyonayo kuhusu yale wanayojifunza, wanafunzi wanaweza kukuza uelewa wao juu ya vitu na masuala ambayo ama yanawasumbua zaidi, au yanawapa hamasa zaidi, au hawayaelewi bado, na kupitia maswali wakaweza kupata ufahamu bora wa ukweli. Kilicho muhimu katika kipindi chako cha darasa ni uwezo wako wa kutengeneza mazingira ambapo wanafunzi wanahisi uhuru wa kuchambua dhana hizi kwa umakini wao wote na kwa kina ambacho wanaweza kukifikia katika mioyo yao na mawazo yao. Katika hatua hii, ni muhimu uwasaidie kuibua masuala na maswali yao wenyewe, na kuyajadili wao kwa wao kwa faida ya kukuza ufahamu wa kina na uzito wa kweli za somo hili. Katika sehemu hii, mifano halisi inalenga katika madai ya kweli ya Neno la Mungu, na jinsi Neno la Mungu linavyoshughulikia masuala yenye utata katika ulimwengu wetu huu wenye mazingira na tamaduni mchanganyiko. Wahimize wanafunzi wasitoe majibu ya papo kwa papo kwa matatizo yaliyoelezwa hapa chini, bali washughulikie masuala hayo kwa namna inayowasaidia kuona jinsi Neno la Mungu linavyotuthibitishia kwa habari ya dhambi, haki, hukumu, na kweli. Kumbuka, mifano halisi huwapa wanafunzi fursa ya kutumia kwa ubunifu katika mazingira halisi kweli ambazo wamejifunza. Zingatia kipengele hiki cha ubunifu katika uongozi wako wa sehemu hii. Sisitiza hapa hitaji la wao kama viongozi kutegemea nguvu ya uthibitisho wa Roho Mtakatifu katika huduma zao binafsi. Ni rahisi kudhani kwamba mahubiri bora, mipango ya kimkakati zaidi, na utendaji wenye malengo zaidi ni mbinu zinazoweza kutumika kwa ufanisi kubadilisha maisha ya wale tunaowaongoza. Kukosa kuelewa kwamba hii ni kazi ya Roho Mtakatifu pekee kupitia Neno la Mungu kunaweza kuzaa aina ya hekima na nguvu ya kidunia katika huduma za
16 Ukurasa 64
Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Mwanafunzi
17 Ukurasa 65 Mifano Halisi
18 Ukurasa 67 Kuhusianisha Somo na Huduma
Made with FlippingBook flipbook maker