Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
/ 1 9 1
U O N G O F U & W I T O
Neno Linalogeuza
MAELEZO YA MKUFUNZI 3
Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi, Somo la 3, Neno Lililogeuza . Lengo la jumla la somo hili la moduli ya Uongofu na Wito ni kuwawezesha wanafunzi wako kuelewa nguvu ya Neno la Mungu inayogeuza, ili kuleta toba, kuzalisha imani, na kusababisha mabadiliko ya maisha. Labda hakuna somo linalohusiana na Maandiko lililo wazi na dhahiri kama uhusiano kati ya Neno la Mungu na nguvu zake za kubadilisha. Kweli hizi zimeunganishwa kwa namna isiyoweza kutenganishwa, na kuliishi Neno ni kupitia mapinduzi ya maisha, kuathiriwa na kubadilishwa kabisa, kwa maneno mengine, kugeuzwa kutoka mfumo mmoja wa maisha na kuingia katika mfumo mpya na tofauti kabisa. Sehemu ya kwanza ya somo hili inaangazia toba na imani, na sehemu ya pili inaangazia ishara na vielelezo vya mtu aliyegeuzwa na Neno. Kama ilivyo katika masomo yetu yote, zingatia kwa umakini malengo mbalimbali ya ufundishaji ambayo utakuwa unayasisitiza katika somo lote. Hakikisha unazingatia kwa umakini malengo haya, yatafakari, na utafute njia mahususi za kuyatilia mkazo katika mijadala yako na wanafunzi. Yesu alilinganisha badiliko linalohitajiwa ili kuingia katika Ufalme wa Mungu na kuzaliwa mara ya pili. Ili kuingia katika utawala wa Mungu ni lazima tugeuzwe, kuzaliwa kutoka juu, si tu matengenezo au juhudi kuelekea utofauti, bali ni maisha mapya kabisa, kufanyika kiumbe kipya (Yohana 1:12-13; Gal. 6:15). Wazo hili (ambalo kimsingi ni wajibu) linafanya mabadiliko makubwa ya kimaadili kuwa sehemu ya msingi wa imani ya Kikristo. Katika usemi huu rahisi Yesu anafafanua upya asili ya imani; si sawa na maadili, mafundisho, taratibu, au desturi. Ni zaidi ya maeneo matakatifu, liturujia, taratibu, au ibada na sherehe za kidini. Ukristo kimsingi unahusu badiliko na uumbaji mpya. Ufahamu huu unaweza kuathiri sana jinsi tunavyoelewa hali yetu ya kiroho, na huduma yetu. Zaidi ya mambo mengine yote, imani ya Kikristo inatafuta upya, uwezo mpya, asili mpya, mwelekeo mpya, na ukweli mpya. Ibada hii inaangazia ukweli huu, ambao unagusa kwenye kiini chenyewe cha mafunzo yetu katika somo hili kuhusu nguvu ya Neno la Mungu inayobadilisha na kufanya upya.
1 Ukurasa 73 Utangulizi wa Somo
2 Ukurasa 73 Ibada
Kama tutakavyojifunza katika somo letu, kila mwelekeo wa nguvu ya Neno inayobadilisha ni wa Mungu – yote tuliyo nayo na ubora wa utu wetu huja kama matokeo ya kuwa na uhusiano sahihi na Mungu kwa njia ya Yesu Kristo. Ni lazima
3 Ukurasa 75
Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi
Made with FlippingBook flipbook maker