Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

1 9 2 /

U O N G O F U & W I T O

tutambue na kusali daima kwamba Mungu, yeye peke yake, aweze kutuandalia msaada na usalama tunaohitaji ili kumtukuza. Kubadilika huku ni kazi ya neema kwa njia ya neema, na ni matokeo ya muungano wetu na Mungu katika Kristo.

Mifano yote katika kipengele hiki inahusu maswala ya ukiri wa imani na uwepo halisi wa imani; ni jambo moja kudai kwamba wewe ni mali ya Mungu katika Kristo, ni jambo lingine kabisa kuwa mali yake katika uhalisia. Jukumu kuu la uongozi wa kiroho katika Kanisa ni jukumu la kubaini na kutofautisha ukiri halisi wa kiroho na maungamo ya uongo ya imani. Mitume walionya kwamba baada ya kifo chao wangejipenyeza katika Kanisa watu wanaodai kuwa wa Kristo, lakini ambao kwa hakika hawakuwa wake hata kidogo (taz. Mdo. 20:29- ; 2 Pet. 2:1-). Kwa wengi wanaojiita Wakristo mijini, imani yao inaweza isiwe imejengwa juu ya msingi wa mageuzi na uongofu wa maisha, bali juu ya imani ya kimafundisho, ushirika wa kijamii, au ushirika wa kitamaduni. Unapofundisha somo hili, itakuwa muhimu kusisitiza changamoto zinazohusiana na kutambua kiroho halisi na imani ya kuigiza. Uongofu si dhana ya Agano Jipya tu; pia imetajwa katika Agano la Kale, hasa kwa wale wanaochukuliwa kuwa wageni au wasafiri kati ya watu wa Mungu. Watu hao walizuiliwa kushiriki katika viwango mbalimbali vya maisha ya kidini ya Waisraeli (Kut. 12:43-45), lakini waliruhusiwa kutoa dhabihu kwa Mungu (ikiwa wametahiriwa), na kuadhimisha Pasaka pamoja na watu wa Mungu (Hes. 14:13 15; Kut. 12:48-49). Ruthu ni mfano dhahiri wa mgeni ambaye “ameongoka” kwa Yehova, na anajumuika pamoja na watu wa Mungu. Taswira inayolingana kwa uwazi zaidi na hii ni taswira ya kinabii inayojulikana sana ya wito wa Israeli kurudi kwa Mungu (k.m., Yer. 3:1-4.4; Isa. 55). Ingawa Israeli hawana imani, (Yer. 3:1 4), Mungu atawahurumia watu wake; anawaita watubu na kupata rehema (Yer. 3:12-13; Isa. 55:1-9). “Uongofu” huu unapaswa kuambatana na ishara zinazotoa ushahidi wa nje wa mabadiliko ya ndani (Yer. 4:1-4). Bila shaka, hakuna dalili ya mabadiliko inayoweza kuzalishwa na Israeli pekee; lazima waimarishwe na nguvu za Mungu mwenyewe (Zek. 4:6; Yer. 3:22), na kufanywa upya kabisa katika uhusiano wao na Mungu na baina ya mtu na mwingine.

 4 Ukurasa 75 Kujenga Daraja

 5 Ukurasa 78 Muhtasari wa Kipengele I

Made with FlippingBook flipbook maker