Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
/ 1 9 3
U O N G O F U & W I T O
Umuhimu wa kuongoka katika Agano Jipya unaweza kuonyeshwa kupitia maisha ya Mtume Paulo, ambaye anaelezea kuongoka kwake kwa lugha ya wito wa kinabii katika Wagalatia 1:15-16. Mabadiliko ya Paulo yalikuja kupitia kukutana binafsi na Kristo mwenyewe, na si tu mabadiliko ya desturi za kidini au kauli za kimafundisho. Mabadiliko yake yalikuwa ni tafakari ya ajabu kabisa na ya kimapinduzi ya ufahamu wake juu ya Mungu, ulimwengu, maisha, wokovu na ukweli kupitia Yesu Kristo. Hata hivyo tunaelewa maneno ya kibiblia, ni wazi kwa kuangalia mfano wa Paulo, kwamba aliongoka kwa maana ya mabadiliko halisi na kamili ya maisha na hali yake. Kabla ya kugeuzwa kwake, alijifafanua kama Farisayo mwaminifu mwenye shauku kubwa kuliko wenzake (Flp. 3:5-6; Gal. 1:14). Baada ya kukutana na Bwana Yesu Kristo aliyefufuka (1Kor. 9:1-2; 15:8-10) Paulo aliongoka mara moja, yaani, kugeuzwa (Flp. 3:7), akapewa wito wa kuwa mtume kwa Mataifa (Gal. 1:15-16) 1Kor. 9:1-2) na mhubiri wa msalaba wa Yesu Kristo (1Kor. 1-2). Maelezo ya pambano la Paulo na Bwana aliyefufuka yamerekodiwa katika Matendo 9, 22, na 26. Picha za uongofu katika Maandiko ni nyingi na zina rangi nyingi: Mungu anawaita wengine kwake (1Kor. 1:2), kununuliwa kwa damu yake (1Kor. 6:20), kuwekwa huru na kukombolewa kutoka katika nguvu za dhambi (Rum. 6:17-18), na wapokeaji wa neema na kibali cha Mungu kisichostahiliwa (Rum. 3:21-26). Katika baadhi ya simulizi (hadithi) juu ya mada ya uongofu katika kitabu cha historia cha Matendo, tunaona uhusiano wa moja kwa moja kati ya kuongoka na imani katika habari njema ya Yesu Kristo. Simulizi muhimu na yenye mpangilio mzuri kuhusu uongofu wa Sauli kuwa Paulo (Matendo 9, 22, 26) inaambatana na simulizi ya kuongoka kwa towashi Mwethiopia (8:26-40) na Kornelio na nyumba yake (10:1-11:18), na wengine wengi ambao waligeuzwa ambao majina yao hatuyajui (k.m., 2:41-42; 4:4; 9:35, 42). Kilicho muhimu katika kutazama simulizi hizi za uongofu ni kwamba mabadiliko ya mtu kuinga katika Ufalme wa Mungu hayatokani na juhudi binafsi, kufanya kazi kwa bidii, au azimio la kimaadili. Wanaume na wanawake waliongoka kutokana na kusikia ujumbe wa upendo wa Mungu katika Yesu Kristo, na kujikabidhi kwao kwake kwa njia ya imani. Tamko hili la kuunganishwa na Mungu kwa njia ya Yesu linathibitishwa kwa njia ya ubatizo, na ishara zinazoambatana za kuzaliwa upya kiroho, ishara za Roho Mtakatifu. Kilicho muhimu kuzingatiwa hapa ni uhusiano wa moja kwa moja kati ya habari njema ya Mungu na Injili. Uongofu hutokea kama matokeo
6 Ukurasa 83 Muhtasari wa Kipengele II-E-2
7 Ukurasa 84
Muhtasari wa Kipengele III-D
Made with FlippingBook flipbook maker