Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

1 9 4 /

U O N G O F U & W I T O

ya kusikia na kuamini Neno la Mungu kuhusu maisha na kazi ya Yesu Kristo, na kukumbatia hadithi hiyo kama kiini cha maisha na uwepo wa mtu. Hakuna jambo tofauti na Injili linaweza kuleta wokovu.

Dhana za sehemu hii ya maswali na majibu zimejikita katika mawazo mengi tofauti lakini muhimu ya kitheolojia ambayo yanalifanya Agano Jipya lote liweze kueleweka. Jadili maswali haya kwa uwazi na kwa muda wa kutosha ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wana ujuzi wa kivitendo wa istilahi muhimu, na uelewa wa maana na matumizi ya istilahi hizo ndani ya duru za kitheolojia. Ingawa uongozi hauhitaji ujuzi wa kiufundi wa misamiati ya kitheolojia, ni muhimu kuelewa maana ya maneno fulani katika muktadha wa kazi ya Mungu katika Kristo kwa ajili ya wokovu wetu. Tumia muda wa kutosha kufafanua dhana hizi. Watake wanafunzi waeleze kwa maneno yao wenyewe maana na upeo wa baadhi ya istilahi maalum zinazotumika katika sehemu hii. Zingatia dhana zilizo nyuma ya istilahi husika, na kile hasa zinachomaanisha pale zinaporejewa katika muktadha wa ufahamu wa kibiblia. Kama ilivyotajwa katika sehemu ya mwisho, asili ya Neno la Mungu ni kuleta mageuzi, kufanya upya na kubadilisha. Uchambuzi wetu wa neno “kuzaliwa upya” ( Palingenesia kwa Kiyunani, kutokana maneno mawili ya Kiyunani yenye maana ya “mpya” na “mwanzo,” “asili, kuzaliwa”) kwa kweli linaonekana mara mbili tu katika Agano Jipya (Mt. 19:28; Tito 3:5). Kama ilivyoelezwa katika sehemu yetu ya mwisho, Agano Jipya linahusisha kwa uwazi Neno la Mungu na kufanywa upya na kugeuzwa, na kwa maana moja, hata ulimwengu wenyewe utajikuta katika mabadiliko wakati wa Ujio wa Pili wa Kristo (au parousia ) (Isa. 65:17-25; 2 Pet. 3:13; Ufu. 21:1). Kwa kuwa nia ya Mungu ni kubadilisha dunia nzima chini ya utawala wa Mungu (yaani, “Tazama, nayafanya yote kuwa mapya” [Ufu. 21:5]), kila kitu kinachohusishwa na Neno linalogeuza kina matokeo ya mara moja (katika wakati wa sasa) na ya kieskatolojia (kinahusishwa na “mambo ya mwisho” ya kurudi kwa Kristo). Hivyo basi, matokeo ya nguvu ya kugeuza ya Neno yote mawili ni ya kibinafsi (k.m., Tito 3:5, 2 Kor. 5:17 - “kiumbe kipya:” Efe. 4:22, 23; taz. Kol. 3:9, 10 – utu “mpya”). Matokeo ya Neno la Mungu linalogeuza ni ya ajabu, na kwa sababu hiyo tunapaswa kutarajia kwamba wale wanaokiri kuunganishwa na

 8 Ukurasa 85 Maswali kwa Wanafunzi na Majibu

 9 Ukurasa 87 Muhtasari wa Kipengele I

Made with FlippingBook flipbook maker