Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
/ 1 9 5
U O N G O F U & W I T O
Mungu kupitia Neno hilo watafanywa upya kibinafsi, kijamii, na kiroho. Maisha haya mapya katika Kristo ni kionjo cha urithi ujao (Efe. 1:13-); ni halisi (ya kibinafsi na ya ndani ya mtu) na ya kijamii (yanaathiri uhusiano wetu na jamii). Wale walioingia katika maisha mapya ya Mungu katika Kristo huingia katika mtindo wa maisha na mwenendo ambao ni tofauti na ulimwengu na yasiyo na muendelezo na mtindo wao wa maisha wa zamani. Vipengele hivi vya upya na kutoendeleza maisha ya kale ndio kiini cha mkazo wa somo hili. Kila mtu aaminiye anaathiriwa kwa njia mpya za ajabu, kulingana na Maandiko, na kuzijua ishara hizi za ndani na za nje ni ufunguo wa kufahamu kuhusu uwepo halisi wa uhai wa kiroho na uwezo wa kubaini udanganyifu mtupu na maungamo ya uongo ya imani. Kutofautisha kati ya “ishara za ndani za wokovu” na “ishara za nje za wokovu” sio suala la kibiblia mara zote na kwa njia nyingi ni suala lisilo na mantiki, lakini linasaidia katika kuelewa asili kamilifu ya mabadiliko ambayo hutokea kwa wale wanaomwamini Kristo. Ni tofauti sahili inayothibitisha kwa uangalifu na kwa nguvu dai la Biblia kwamba wale wanaoongoka kwa Neno wanapitia uumbaji mpya katika hali zao za ndani (yaani, akili zao, nafsi, roho, haiba) pamoja na mahusiano yao na Mungu, na wengine, na hasa wale ambao pia wameunganishwa na Kristo katika imani, washirika wanaoitwa “Kanisa” (k.m., Mdo. 2:42-47; 1 Kor. 12:13; Warumi 12:4-8). Katika sehemu hii ya maswali kwa wanafunzi na majibu, unapaswa kuzingatia kile ambacho Neno la Mungu linafundisha kuhusu ishara zinazopaswa kuambatana na imani ya kweli katika Yesu Kristo. Ishara za ndani na za nje za wokovu zimeunganishwa moja kwa moja na Neno la Mungu, na sehemu kubwa ya wajibu wa kiongozi wa kiroho ni kuwasaidia wengine kuelewa na kuakisi maisha mapya yanayohusiana na kumjua Kristo kama mfuasi wake. Zingatia kwa makini dhana zinazotokana na maswali haya, ambayo yamekusudiwa kuibua yale unayoweza kutaka kujadili unapofanya marudio ya maudhui ya somo katika sehemu ya pili ya video.
10 Ukurasa 89 Muhtasari wa Kipengele II
11 Ukurasa 92 Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
Made with FlippingBook flipbook maker