Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
1 9 6 /
U O N G O F U & W I T O
Unapopitia dhana mbalimbali zinazohusishwa na somo hili hakikisha kwamba unaangazia istilahi zozote muhimu zilizojitokeza katika sehemu ya kwanza, hata unapofanya mapitio ya mawazo yaliyoelezwa katika sehemu ya pili ya video. Kuhusiana na nguvu za Neno la Mungu katika ujumla wake, somo hili ni muhimu kwa maendeleo ya uongozi, kwani limejikita kwenye msingi wa maisha ya kiroho halisi. Injili ya Yesu Kristo inageuza – inabadilisha. Unapopitia dhana hizi hakikisha kwamba unaelezea kwa mara nyingine tena kweli zinazoangazia eneo hili muhimu la Neno la Mungu. Mifano hii imekusudiwa kuonyesha baadhi ya matatizo ya kawaida yanayohusiana na kweli hizi. Kilicho muhimu unapowaongoza wanafunzi katika mjadala wa wazi ni namna unavyowawezesha kutambua masuala na maswali yanayotokana na kutafakari juu ya uwezowa kugeuza uliomo katikaNeno laMungu. Kama viongozi, watalazimika kuona kwamba inahitaji ustadi mkubwa, uwazi, na unyenyekevu wa hali ya juu ili kutumia Neno la Mungu kwa usahihi katika hali fulani. Tunachopaswa kutafuta hapa ni kujitoa kwa dhati kushughulikia mambo kwa kuzingatia kweli za Biblia, bila kutafuta matumizi ya kipekee ya kanuni fulani ya kibiblia, ambayo tunadhani kuwa ndiyo ukweli usiopingika. Kadiri wanafunzi wanavyoshiriki katika kujadili mifano hii ndivyo watakavyokumbana na changamoto zinazohusiana na kanuni ya “kupambanua mema na mabaya” kama ilivyotajwa katika Waebrania 5:11-44. Tumia mifano hii kuwasaidia wanafunzi kukabiliana na mazingira halisi ya kivitendo ya kweli wanazojifunza. Unaposafiri na wanafunzi wako katika kina cha Neno la Mungu, inaweza kutokea kwamba baadhi ya wanafunzi wako wanatatizika na matumizi au uelewa wa baadhi ya vipingele vinavyohusiana na Neno na nguvu zake za kubadilisha. Jambo muhimu katika kusaidia ugunduzi wao ni uwezo wako wa kuwatia moyo, kuwapa usaidizi na mwelekeo mara kwa mara. Kama mshauri, jukumu lako si lazima kujibu kila swali ambalo wanaweza kuwa nalo (kimsingi hungeweza kufanya hivyo!). Badala yake, unapaswa kuwaelekeza kwenye Maandiko kama nyenzo ya msingi ya kujifunza Biblia na theolojia, pamoja na mapokeo yenye utajiri wa maarifa ya makanisa yanayoamini Biblia. Katika yote tunayotoa kama ushauri, itakuwa muhimu kutoa ushauri endelevu na maombi ya wazi na yaliyojaa imani
12 Ukurasa 93 Muhtasari wa Dhana Muhimu
13 Ukurasa 95 Mifano Halisi
14 Ukurasa 97 Ushauri na Maombi
Made with FlippingBook flipbook maker