Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
/ 1 9 7
U O N G O F U & W I T O
kwa wanafunzi wetu wanapojiandaa kuingia katika viwango vya kina vya huduma. Chukua muda uwezavyo, ama wakati wa vipindi vyako au nyakati zingine, kuendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo ya wanafunzi, ukiwashauri kutafuta njia za kutumia Neno la Mungu katika maisha na huduma zao.
Huu sasa ni wakati muhimu wa masomo kwa moduli hii. Kufikia mwisho wa kipindi cha pili cha somo hili, unapaswa kuwasisitiza wanafunzi umuhimu wa kuwa wamefanya kazi ya msingi na kufikiria kwa usahihi jinsi wanavyokusudia kutekeleza Kazi ya Huduma kwa vitendo. Kadiri wanavyofanya maamuzi mapema zaidi kuhusu kile wanachotaka kufanya katika kazi zao, ndivyo wakavyokuwa na muda mzuri na wakutosha zaidi kupanga na kutekeleza kazi zao. Pia, kufikia wakati huu, unapaswa kuwa umehimiza kila mwanafunzi kuchagua kifungu atakachosoma kwa ajili ya Kazi ya Ufafanuzi wa Maandiko (eksejesia). Kazi ya Huduma na Kazi ya Ufafanuzi itakamilika kwa ubora zaidi kadri wanafunzi watakavyoamua mapema kile wanachotaka kufanya na kufikiria jinsi watakavyokikamilisha. Wakumbushe juu ya maandalizi haya ya mapema, kwa kuwa, kama ilivyo katika masomo yoyote, mwishoni mwa kozi kunakuwa na mambo mengi yanayopaswa kukamilishwa, na wanafunzi wataanza kuhisi shinikizo la kudaiwa kazi kadhaa kwa wakati mmoja. Njia yoyote ambayo unaweza kutumia kuwakumbusha juu ya umuhimu wa kujipanga mapema itakuwa ya manufaa kwao, kwamba wanatambua hilo au la. Kwa sababu hii, tunashauri kwamba ufikirie kukata maksi kadhaa kwenye kazi zitakazo kusanywa kwa kuchelewa. Ingawa kiwango cha maksi za kukatwa kinaweza kuwa cha kawaida, utekelezaji wako wa kanuni ulizojiwekea utawasaidia kujifunza kuwa makini, wenye ufanisi na kujali muda wakati wanapoendelea na masomo yao.
15 Ukurasa 98 Kazi
Made with FlippingBook flipbook maker