Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

/ 1 9 9

U O N G O F U & W I T O

Neno Linaloita

MAELEZO YA MKUFUNZI 4

Karibu katika Mwongozo wa Mshauri wa Somo la 4, Neno Linaloita . Hili ni somo la mwisho katika moduli ya Uongofu na Wito, na limeandaliwa kwa kusudi la kuwawezesha wanafunzi wako kuelewa asili ya Neno la Mungu katika kutuita kuishi aina ya maisha yanaoendana na uumbaji wa maisha yetu mapya katika Kristo, uthibitisho wetu wa kina kuhusu kweli katika Kristo, na uongofu wetu mpya katika Kristo. Wito huo umejikita katika tabia ya maisha yetu ulimwenguni, ukielezea kwa undani uhusiano wetu na Mungu katika Kristo, mapambano yetu na Shetani na nguvu zake za giza, na mahusiano yetu na Waamini wengine. Kutokana na wingi wa mambo ambayo yameangaziwa katika moduli hii, itakuwa muhimu maradufu kuzingatia malengo kama mwongozo na muhtasari wa utafiti wako katika somo la Neno. Malengo yaliyo hapa chini yanaangazia kweli muhimu zinazohusishwa na Neno Linaloita , na kama unavyojua tayari, jukumu lako kama Mshauri ni kuwezesha majadiliano na uchanganuzi wa dhana hizi katika kipindi chote cha somo, hasa wakati wa mijadala na wanafunzi. Malengo yanaweza kukuwezesha kuwa na aina fulani ya muhtasari wa kweli kuu zinazojadiliwa katika somo zima. Kama watu ambao tumejitoa wenyewe kuishi kweli ya Ufalme wa Mungu kupitia Neno la Yesu Kristo, tuko kwenye safari, misheni, agizo. Bila kujali namna mambo yanavyoonekana, mfumo huu wa ulimwengu wa sasa hauwakilishi utawala na kusudi la Mungu, na kama wanafunzi wa Yesu tunapewa changamoto ya kuishi katika hali ya kutoendana na ulimwengu, tunahesabiwa kuwa ni watu wa uraia tofauti, na tunangojea kufunuliwa kwa mji mpya (Flp. 3:20; Ebr. 11:10). Hivyo ndivyo tulivyo, kama vile nyimbo za zamani zilivyosimulia, “wa kupita tu” na “dunia hii sio nyumba yangu.” Wito wa ufuasi ni wito wa kuakisi mfumo mbadala wa maisha, kusudi la tofauti, njia isiyo na wasafiri wengi. Ibada hii inalenga katika msimamo thabiti ambao tumeitiwa wa kutoendana kabisa na dunia, na inatoa utangulizi fasaha kwa somo letu la leo la kuitwa na Mungu, kuitwa kutoka ulimwenguni.

 1 Ukurasa 101 Utangulizi wa Somo

 2 Ukurasa 102 Ibada

Maombi hayani hitaji la ujasiri na uamsho, ambaonimuhimukwawalewanaotamani kuishi kulingana na kusudi kuu na wito wa kibiblia unaotokana na imani katika Yesu Kristo. Tunamwomba Mungu atupe ujasiri, kwa sababu ni wale tu walio na ujasiri wa kushikilia kweli ya Yesu Kristo wanaoweza kuakisi maana kamili ya

 3 Ukurasa 103

Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi

Made with FlippingBook flipbook maker