Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

2 0 0 /

U O N G O F U & W I T O

Ufalme tunaouwakilisha na kuudhihirisha. Tunaomba uamsho kwa ajili ya nguvu za Roho Mtakatifu pekee zinazoweza kuwawezesha wale wanaomtumikia Mungu katika majiji kuwa na ufanisi katika ushuhuda wao juu ya Kristo katikati ya giza la kiroho na uasi. Kwa wale walio makini kuhusu kutimiza wito wa Mungu, ni maombi yenye bidii tu, yaliyojaa imani ambayo yatatosha kutupa nguvu za rohoni za kustahimili changamoto tunazokabiliana nazo tunapotembea na Bwana. Ni Mungu pekee anayeweza kutufanya watenda kazi halali kwa kusudi na maono ya ufalme wake, na ni maombi pekee yanayoweza kutuunganisha na nguvu zake. Ingawa ni makosa kabisa kuutafsiri wito wa mtu katika maana finyu ya mwenendo wa kimaadili na juhudi za kibinadamu, si hoja ndogo pia kwamba kuwa Mkristo ni kuakisi maana ya kuishi kama mtu wa Mungu katika ulimwengu. Kuna masuala mengi muhimu ya kimaadili yanayotokana na kujitoa kwa dhati kuishi wito wa Mungu mjini. Mifano inayotolewa katika kipengele hiki cha kujenga daraja na kile cha mifano halisi cha somo hili imekusudiwa kuwapa wanafunzi taswira ya mapambano na migongano iliyopo kati ya kuishi imani yetu kwa uadilifu na kushindana na maamuzi ambayo yanatufanya tuhatarishe imani hiyo. Ili kuwa wanafunzi na wafanya-wanafunzi wenye matokeo, ni lazima tutafute njia za kuishi katika misingi ya imani yetu, kujengwa katika hekima bora zaidi inayotokana na Maandiko yanayofundishwa na Roho Mtakatifu, na hekima inayotokana na ushauri wa kimungu ndani ya Mwili wa Kristo. Changamoto yetu ni kutambua mapenzi ya Mungu katikati ya hali tunazopitia ili kuziwezesha familia na makanisa yetu kuishi maisha yanayodhihirisha utajiri wa wito tulionao katika Mungu. Unapotafakari juu ya mifano mbalimbali katika somo hili, tafuta kuwasaidia wanafunzi wako kufafanua uhusiano kati ya wito wa mamlaka wa Kristo na maamuzi mahususi ambayo wale wanaohusika wanatakiwa kuyafanya katika kila hali na kila mazingira wanayokutana nayo. Lugha ya Agano Jipya kuhusu ufuasi inaweka wazi kwamba ufuasi unahusika na uhusiano wa karibu na Yesu Kristo mwenyewe. Neno la Kiyunani linalotafsiriwa na neno “mwanafunzi” halitokei kama maana kuu ya “ufuasi” katika Agano Jipya. Kitenzi “kumfanya mtu kuwa mfuasi” hakionekani sana pia. Neno la “mwanafunzi” linapatikana mara 261, na zote hizo ni katika Injili na Matendo

 4 Ukurasa 104 Kujenga Daraja

 5 Ukurasa 106 Muhtasari wa Kipengele I

Made with FlippingBook flipbook maker