Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
/ 2 0 1
U O N G O F U & W I T O
ya Mitume. Mkazo wa wazi unaonekana kuwa katika Injili, huku asilimia 90 ya matumizi yote ya neno hilo yakitokea katika Injili. Kitenzi cha Kiyunani akolouthein ambacho kimantiki kinamaanisha “kutembea nyuma ya~, kufuata,” kinafafanua kile ambacho mwanafunzi hufanya na jinsi mfuasi anavyokuwa. Kati ya nukuu zake 90, 79 zinapatikana katika Injili, na nyingine katika Matendo (4), Ufunuo (6), na 1 Wakorintho (1). Idadi kubwa ya nukuu za neno hili katika Injili inadhihirisha uhusiano huu wa karibu kati ya Yesu mwenyewe na dhana nzima ya ufuasi. Katika majadiliano yako na wanafunzi, utahitaji kujadili vipengele vya ufuasi vinavyohusishwa na uhusiano wa dhati na Yesu Kristo. Asili ya ufuasi kama Neno linaloita inahusu kuanzishwa kwa uhusiano mpya na wa msingi na Mungu kupitia Yesu Kristo. Akiwa Bwana wa wote na Mwana wa Mungu, Yesu sasa anazo sifa zote za kuwekea masharti maisha ya wanafunzi wake. Wakiwa wawakilishi wake wanaofuata mafundisho yake sawasawa na kwa uwazi, lengo lao ni kumpendeza yeye katika mambo yote, na kupitia ushirika wao pamoja naye kustahimili lolote linalohitajiwa ili kumpendeza na kumtukuza; lengo lao ni kufanana naye katika mambo yote (taz. Lk. 6:40). Ufuasi unahusisha kuishi kwa ajili ya kile ambacho Yesu anaamua na kuelekeza, kutafuta kuakisi kile anachotaka na alichotuita ili tuwe. Kama watu wake, tumeitwa kuvunja itii wowote kwa ulimwengu wa uovu (1 Yoh. 2:15-17), kuwa pamoja naye na kuhubiri Habari Njema (Mk. 3:14), na kuhusishwa kabisa na mateso yake na Ufalme wake (Mt. 6:33). Kama vuguvugu ambalo msingi wake ni Yesu, wito huo unahusishwa kimsingi na wito wa kimishenari wa kufanya mataifa yote kuwa wanafunzi, na kwenda kama kundi la wanafunzi waliotumwa. Watu wa Yesu wana ushirika naye na Ufalme wake, na wanatafuta kupanua utawala wake kupitia kazi ya kufanya wanafunzi. Wito wa kumfuata Yesu wakati huo huo ni wito wa kuacha ulimwengu, kuachana kabisa na mambo yaliyopita, tukiwa na tumaini la kutimiza wito wetu wa kufanya wanafunzi hadi kuja kwake mara ya pili katika utukufu (Mt. 28:18-20).
6 Ukurasa 109 Muhtasari wa Kipengele II
Maswali haya yote yanaunganishwa na wito wa ufuasi, kina cha uhusiano unaobubujika kutoka katika kutembea kwetu na Mungu kupitia Yesu Kristo. Unapojadili haya na wanafunzi, hakikisha kwamba unawekea mkazo wazo kwamba kiini cha ufuasi ni uhusiano tunaoanzisha na kukuza katika Yesu – yeye ndiye
7 Ukurasa 111 Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
Made with FlippingBook flipbook maker