Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

/ 2 0 3

U O N G O F U & W I T O

“Kutoka” kwa ajili ya Israeli iliyorejeshwa, ya eskatolojia. Kuna uhusiano wa moja kati ya watu wa Mungu wa Agano la Kale na mtazamo wa Agano Jipya wa jumuiya ya Kikristo. Uelewa wa Yesu juu ya Kanisa lake, ambalo milango ya kuzimu haingelishinda (Mt. 16:18), hautofautiani, kwa hiyo, na dhana ya Agano la Kale ya watu wa agano wa Mungu. Kinachoshangaza kweli kweli katika mafundisho ya mitume kuhusu jumuiya ya Kikristo, hata hivyo, ni kujumuishwa kwa Wamataifa katika ahadi ya agano la Ibrahimu (taz. Rum. 16, Efe. 3, na Kol. 1:25-). Wazo hili la kujumuishwa kwa Wamataifa kwa imani katika ahadi ya agano la Ibrahimu hakika haliendani na dhana ya jumuiya ya wakati wa Yesu na Mitume (yaani, Mafarisayo, Waesene, Wazeloti, Masadukayo), ambao waliona mataifa ya Kiyahudi kwa namna fulani kama ya pekee, na yenye upendeleo kama watu wa kipekee wa agano wa Mungu. Kujumuishwa huku kunawakilisha ufunuo wa kina na wenye utajiri zaidi wa dhana ya jumuiya kuliko ambavyo ungeweza kukubaliwa na kueleweka na watu wa zama za Mitume. Kama Bwana, Yesu ndiye kichwa cha jumuiya mpya ya wanafunzi wanaomkumbatia kama Neno la mwisho la Mungu kwa wanadamu (Ebr. 1:1-4), na nafsi yake kama kielelezo cha mwisho cha matakwa yote ya Mungu (Kol. 2:6-7). Yeye ambaye sasa ni Bwana, ndiye mwanzilishi wa vuguvugu la wale walioitwa kutoka ulimwenguni (Lk. 9:57-62) kumjia Mungu kama Upendo mkuu na Mungu kamili (Mt. 6:24; taz. 4:9-10). Kwa hiyo, hakuna mtu anayeweza kudai kuwa ameitwa amjie Kristo na kupuuza ukweli kwamba wito huu vilevile ni wito wa kuingia katika jumuiya, wito wa kufanyika mshirika wa watu wa Mungu, na pia wito wa kuwa mali ya Kristo. Ni kitu kimoja (rej. Mdo. 2:39-47). Neno kuhusu uhuru limefafanuliwa kwa uwazi katika Agano Jipya, hasa nyaraka za Paulo ambazo zinalenga katika ufahamu wa kipekee wa kiini cha imani ya Kikristo kama uhuru. Paulo ana mwelekeo wa kufikiria uhuru hasa katika maana yenye sehemu tatu: uhuru mbali na Sheria, uhuru mbali na utumwa wa dhambi, na uhuru mbali na kifo. Kiini cha ufahamu huu wa Ukristo kama uhuru kinatiririka kutoka katika ufahamu wa Paulo kwamba Kristo anatosha kikamilifu kushughulikia masuala yote yanayohusiana na makundi haya matatu. Kama haki yetu, Kristo ametuweka huru mbali na hukumu ya Sheria (2Kor. 5:18-21); kama nguvu zetu, ametuweka huru mbali na nguvu, adhabu, na uwepo wa dhambi (Rum. 6:1-11); na, kama uzima wetu, Yesu ametuweka huru mbali na sheria ya dhambi na mauti (Rum. 8:1-4).

 9 Ukurasa 116 Muhtasari wa Kipengele II

Made with FlippingBook flipbook maker