Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
2 0 4 /
U O N G O F U & W I T O
Neno linalotuita kwenye uhuru linatuita kwenye uhusiano wa karibu sana na Yesu ambao unaturuhusu kuishi kiwango cha maisha ambayo ni yeye pekee anayeweza kudhamini na kuyafanya kuwa mazuri. Kila kinachotufanya kuwa watumwa, ikijumuisha vifungo vya ndani, majaribu ya nje, na upinzani wa kipepo, vinashindwa kikamilifu katika Kristo, ambaye ndiye pekee aliyetuweka huru (Gal. 5:1). Ujasiri tulio nao katika uweza wa Kristo kukomboa ni msingi mkuu wa huduma ya mijini. Silaha za vita vyetu na asili ya huduma yetu ina msingi wake katika ukombozi, kwa sababu Kristo alikufa na kufufuka ili kuwakomboa kikamilifu wale ambao wamekandamizwa sana na makosa, maumivu, kupuuzwa, na taabu (Luka 4:16). Hakuna maelezo yoyote yanayotosha kuonyesha jinsi ukweli huu ulivyo muhimu kwa wale wanaoishi na kuhudumu katika majiji, ambayo yanaweza kusemwa kuwa ni mizinga ya utumwa na ukandamizaji. Kazia ukweli huu muhimu katika mjadala wako kuhusu uhuru wakati wa somo hili. Utume wa Kanisa mara nyingi umefupishwa katika aya ya Injili inayojulikana kama “Agizo Kuu” la Yesu Kristo, lililoandikwa katika Mathayo 28:18-20. Hili ndilo tukio mashuhuri zaidi kati ya yote katika simulizi za baada ya Ufufuo katika Injili na Matendo ambapo Yesu anasemekana kuwaelekeza jumuiya yake ulimwenguni kufanya utume kwa jina lake (Mk. 16:15; Luka 24:47-49; Yoh. 20:21-21-23; Matendo 1:8). Yesu kama Bwana aliyefufuka na aliye hai ameliamuru Kanisa lake (Mt. 16:18) kufanya mataifa yote kuwa wanafunzi na kufanya hivyo hadi mwisho wa dahari, wakati ambapo yeye mwenyewe atarudi (Mt. 28:20). Ushuhuda wa Yohana kuhusu Agizo la Utume wa Kristo umeandikwa katika sura ya 20 ambapo Yesu anasema “Kama vile Baba alivyonituma mimi, nami nawatuma ninyi.” (Mst. 21). Hii inaonyesha kwamba utume si suala la kiisimu tu; lengo hapa ni kuona kwamba Kanisa, kupitia kutimizwa kwa utume wake duniani, kwa kweli linapanua na kuendeleza huduma ya Yesu ulimwenguni, kwanza kupitia wanafunzi wake na kisha kupitia Kanisa (ms. 19, 20). Kwa hiyo, maelezo ya Yohana yanasema kwamba kwa namna ileile ambayo Baba alimtuma Mwana ulimwenguni kama umwilisho wa maisha yake (Yohana 1:14-18), ndivyo Kanisa linapaswa kwenda ulimwenguni likiakisi maisha ya Yesu katika upendo (Yoh. Yoh. 13:34-35), kutoa msamaha wa dhambi (mst. 23), likitumwa kwa uwezo na mamlaka ya Yesu (mst. 21) katika nafsi na nguvu za Roho Mtakatifu (mst. 22).
10 Ukurasa 119 Muhtasari wa Kipengele III
Made with FlippingBook flipbook maker