Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
/ 3 5
U O N G O F U & W I T O
MUUNGANIKO
Somo hili linaangazia baadhi ya vipengele muhimu vya uwezo wa uumbaji wa Neno la Mungu, kwa ukamilifu katika uumbaji wa ulimwengu, na kidhamira, katika uumbaji wa maisha mapya ya kiroho ndani ya moyo wa mwamini. Kwa kila namna, wazo la Neno la Mungu ni muhimu kwa kuelewa kazi ya Mungu ulimwenguni, na katika historia yote ya mwanadamu. ³ Maandiko Matakatifu ni Neno la Mungu lililo hai na la milele. Yametiwa uzima wa Mungu mwenyewe kupitia uvuvio wake, na pia yanahusishwa moja kwa moja na nafsi ya Mungu na kazi yake. ³ Kwa sababu Maandiko yanahusishwa kwa karibu sana na nafsi na kazi ya Mungu, kwa hiyo ni ya kutegemewa kabisa na yenye mamlaka kabisa kwa habari ya masuala yote ya imani katika kila kitu ambacho yanasema kuwa ni kweli. ³ Ulimwengu wote mzima na uhai wote uliomo uliumbwa “ ex nihilo ” (yaani, pasipo kitu chochote) kwa nguvu zinazotoa uhai za Neno la Mungu, yaani, kwa maneno aliyotamka wakati wa uumbaji. Zaidi ya hayo, Mungu Mwenyezi aliumba vitu vyote kwa njia ya Neno Hai, Yesu Kristo (Yohana 1:1-3; Kol. 1:16). ³ Maandiko ni Neno “kauli” la Mungu, lililovuviwa na Roho, na linajumuisha Agano la Kale (yaani, Maandiko ya Kiebrania) na Agano Jipya (yaani, Maandiko ya Kikristo). ³ Mungu anajitambulisha kikamilifu na Neno-mtu la Mungu, Yesu Kristo, ambaye kupitia kwake Mungu amejifunua mwenyewe, anaukomboa ulimwengu, na atarudisha ulimwengu wote mzima chini ya utawala wake wa haki. ³ Neno la Mungu, likiwa limeletwa na Roho Mtakatifu na hivyo kubeba uzima wa Mungu mwenyewe, ni chombo muhimu ambacho kupitia hicho maisha mapya yanaumbwa kwa wale wanaomwamini Yesu. Ujumbe wa Injili ni mbegu ya kiroho inayotufanya tuzaliwe kutoka juu. ³ Ishara halisi ya ufuasi wa kweli katika Kristo ni kukaa na kuendelea katika Neno la Yesu, ambalo huwaweka huru waamini. ³ Mungu amempa kila mwamini Roho Mtakatifu ili tuweze kuelewa na kufahamu maana ya Maandiko ambayo aliyavuvia (1Kor. 2:9-16 linganisha na 2 Pet. 1:21-22). ³ RohoMtakatifu anatufundisha kwamba kusudi kuu la ulimwenguulioumbwa ni kumtukuza Mungu Mwenyezi (Isa. 43:7; Mit. 16:4; 1 Kor. 10:31).
Muhtasari wa Dhana Muhimu
ukurasa 180 10
1
Made with FlippingBook flipbook maker