Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
3 6 /
U O N G O F U & W I T O
³ Maandiko, Neno linaloumba, hutuwezesha kumtukuza Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu tunapoishi chini ya utawala wa Mungu.
Sasa ni wakati wa wewe kujadili pamoja na wanafunzi wenzako maswali yako kuhusu nguvu ya Neno linaloumba. Je, una maswali gani hasa kwa kuzingatia maarifa ambayo umejifunza hivi punde? Pengine maswali yaliyo hapa chini yanaweza kuibua mjadala wenu pamoja, na kukusaidia kuunda maswali yako mwenyewe, mahususi na muhimu zaidi. * Tunaposema kwamba Maandiko yamevuviwa na Mungu, je, tunamaanisha “hati asilia” (yaani, hati ambazo manabii na Mitume waliandika), tafsiri, nakala za tafsiri, au kila kitu? * Imani yetu ya kwamba Mungu aliumba ulimwengu kupitia Neno lake ina matokeo gani kuhusiana na mjadala juu ya nadharia ya mageuzi ( evolution )? Je, nadharia ya mageuzi ni jambo tunalohitaji kuhangaikia au la? * Ikiwa Neno la Mungu li hai na lina nguvu na uwezo wa kuumba, kwa nini halionekani kufanya kazi namna hiyo katika moyo wa kila mtu anayelisikia? Kwa nini watu wengi sana wanaukataa ujumbe wa Neno leo? * Je, kuna uhusiano gani hasa kati ya Neno la Mungu katika Yesu na Neno la Mungu katika Maandiko? Lipi linapaswa kupewa uzito zaidi ya lingine? Au je, yamekusudiwa kuchukuliwa na kuheshimiwa kwa kiwango sawa? * Je, tunapaswa kuhusianaje na Roho Mtakatifu, kivitendo, ili tuweze kujua kwa hakika kwamba atatufundisha tunapojifunza Neno la Mungu? * Ikiwa nitajifunza Neno la Mungu katika muktadha wa kusanyiko, kuna umuhimu gani wa kuwa na muda wangu binafsi wa kujifunza Neno la Mungu? Je, ikiwa sikubaliani na baadhi ya mambo ambayo yanafundishwa katika kanisa langu, au na mchungaji wangu – nifanyeje?
Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Mwanafunzi
ukurasa 180 11
1
MIFANO
Kesi Nzito ya Kutoelewana
Wakati kanisa fulani limekuwa na mfululizo wa mafundisho juu ya Ujio wa Pili wa Kristo, binti mmoja ambaye ni kiongozi kijana wa Kikristo amekumbana na mafundisho katika mahubiri ya mchungaji ambayo hayaelewi, na, kwa mtazamo wa haraka haraka, hakubaliani nayo. Ametumia muda fulani kujadiliana na mchungaji baadhi ya mambo hayo ambayo kijana huyo anapingana nayo, na hakuna hata moja kati ya hayo ambalo ni la msingi sana, kwa maana ya kwamba linakinzana na
1
ukurasa 180 12
Made with FlippingBook flipbook maker