Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
3 8 /
U O N G O F U & W I T O
anaelewa kwamba Roho Mtakatifu alikuja na kukaa ndani yake na kumtia muhuri mara tu alipoamini (k.m., Rum. 8:1-18; Efe. 1:13; Gal. 5:16-23), hajui maana ya “kufundishwa” na Roho takatifu. Haamini sana kwamba anapaswa kupitia mazoezi mengi ya kihisia ili kusema kwamba anafundishwa na Roho, na kila mtu anamtambua ndugu huyu mpendwa kuwa ni mtumishi aliyekomaa, mcha Mungu, na mwenye kumfanania Kristo katika kanisa. Bado, anataka kuelewa maana ya kufundishwa na Roho. Je, ungewezaje kumfundisha ndugu huyu kuelewa utendaji wa huduma ya kufundisha ya Roho Mtakatifu katika jitihada zake za kuendelea kujifunza Biblia? Maandiko Matakatifu ni Neno la Mungu, rekodi iliyoandikwa ya Neno la Bwana lenye uzima na la milele. Kwa sababu yamevuviwa na Roho Mtakatifu (kihalisi, pumzi ya Mungu) ni ya kuaminiwa kabisa na ya kutegemewa katika yote yanayosemwa ndani yake. Neno la Mungu hutupatia kusudi la Mungu la milele juu ya uumbaji, yaani, kwamba vitu vyote vilifanywa kupitia Neno la Mungu liumbalo na linaloleta uhai kwa utukufu wake mkuu. Bwana Mungu anajitambulisha kikamilifu katika Neno la Mungu kwa njia ya Yesu Kristo. Yeye ndiye ambaye kupitia kwake Mungu anajifunua kwetu, anaukomboa ulimwengu, na atarudisha ulimwengu wote chini ya utawala wake wenye adili. Neno hili, kwa njia ya Roho Mtakatifu, hutengeneza maisha mapya ndani ya wale wanaoamini. Ufuasi wa kweli ni kudumu katika Neno hili katika Kanisa, ambalo huzaa ndani ya mwamini ukomavu wa kiroho, kina, na ukuaji katika kusudi na mapenzi ya Mungu. Iwapo ungependa kufuatilia baadhi ya mawazo ya somo hili la Neno Linaloumba , unaweza kujaribu vitabu vifuatavyo: Fee, Gordon D. na Douglas Stuart. How to Read the Bible for All its Worth . Grand Rapids: Zondervan, 1982. Montgomery, John Warwick. God’s Inerrant Word . Minneapolis: Bethany Fellowship, 1973. Sproul, R.C. Knowing Scripture . Downers Grove: InterVarsity, 1977. Tenney, Merrill. The Bible: The Living Word of Revelation . Grand Rapids: Zondervan, 1968.
1
Marejeo ya Tasnifu ya Somo
Nyenzo na Bibliografia
Made with FlippingBook flipbook maker