Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
/ 4 3
U O N G O F U & W I T O
Neno Linalothibitisha
S O M O L A 2
ukurasa 183 1
Karibu katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma, kujifunza, kushiriki katika mijadala, na kutendea kazi yaliyomo katika somo hili, utaweza kueleza na kutetea kwa kutumia Maandiko ukweli kwamba: • Neno la Mungu ndilo Neno linalothibitisha kuhusu dhambi, haki, na hukumu. • Kati ya njia zote tunazoweza kumwelewa Mungu na kuielewa kazi yake, ni Neno la Mungu katika Maandiko linalotuwezesha kuielewa dhambi – kwamba ni ya ulimwengu wote katika upeo wake na ina asili ya uharibifu. • Sheria ya Mungu hututhibitishia kwa habari ya dhambi zetu, ikifunua umbali kati ya matendo na nia zetu na matakwa matakatifu ya Mungu. • Neno la Mungu huthibitisha kuhusu haki, likiweka wazi kupungua kwetu katika kushika Sheria ya Mungu, na kuifunua haki ya Mungu kwa imani kupitia kifo na ufufuo wa Yesu Kristo. • Neno la Mungu linathibitisha kuhusu hukumu, likifunua nia ya Mungu ya kuhukumu viumbe vyote kila mahali, na hukumu yake inayokuja juu ya Israeli na mataifa, juu ya Kanisa, juu ya Shetani na malaika zake, na wafu wote waovu. • Neno la Mungu huthibitisha kuhusu asili ya ukweli, yaani, yaliyo ya kweli kumhusu Mungu, kazi yake ulimwenguni, na hatima na kusudi la wanadamu. • Neno la Mungu pia huthibitisha kuhusu mada kuu ya Maandiko: ufunuo wa nafsi na kazi ya Yesu Kristo. • Neno la Mungu pia linathibitisha kuhusu usuli mkuu wa ufunuo wote wa Mungu: ufunuo wa mpango wake wa ufalme. • Neno la Mungu huthibitisha kupitia uadilifu wa wajumbe waliochaguliwa na Mungu, manabii na Mitume, ambao walipewa kazi ya kumwakilisha Mungu, kuzungumza juu yake na kuufafanua mpango wake.
Malengo ya Somo
2
Made with FlippingBook flipbook maker