Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
4 4 /
U O N G O F U & W I T O
Baraka ya Huzuni
Ibada
Soma Zaburi 32:1-11 . Je, umewahi kuhangaika na dhamiri yenye hatia? Si hatia ya uongo, kumbuka, bali kule kujua moyoni mwako kwamba ulifanya kitu kibaya, na unahisi vibaya juu ya kile ulichokifanya – na ungetamani kutengeneza, kutatua, kuweka mambo sawa na mtu uliyemuumiza? Hisia hii ni mojawapo ya hali za ndani zenye afya zaidi unazoweza kuwa nazo. Ingawa inaweza kuonekana kuwa ni hisia ya huzuni na ngumu, au hata ya aibu, hisia ya kuhukumiwa moyoni kwa sababu ya makosa yako, na kile ulichokifanya, ni mojawapo ya hisia muhimu zaidi kuwa nazo. Hapana shaka juu hilo; hali hii ya kuhukumiwa, ya kuhisi hatia yako mwenyewe mbele za Mungu katika dhamiri yako, inahusishwa na hisia. Kwa kweli, mtu anayefanya makosa na hajali, hana hisia ya kuwajibika au kujilaumu ndani yake, yuko katika shida kubwa ya kiroho. Kukosa uwezo wa kuhukumiwa na Mungu kunakufanya uwe katika hatari ya kufanya mabaya bila hisia ya toba, huzuni, au nia ya kubadilika. Daudi katika zaburi hii anazungumza moja kwa moja juu ya uwezo wa Mungu wa kusamehe, na hisia yake mwenyewe ya maumivu na aibu wakati alipochelewesha toba yake na kurudi kwa Bwana. Taabu tunayohisi wakati Roho Mtakatifu anatuthibitishia juu ya dhambi zetu ni aina iliyobarikiwa ya taabu, tofauti na aina nyingine zote za mapambano au maumivu ya ndani. Taabu hii inaweza kutuwezesha kuelewa makosa yetu wenyewe, kiwango cha Mungu cha haki, kutoweza kwetu kusimama katika kweli ya Mungu kwa nguvu zetu wenyewe, na deni letu kwa Mungu kutokana na makosa ambayo tumefanya. Taabu hii inatuongoza kwenye ukweli kuhusu sisi wenyewe na kuhusu Mungu; tutakuwa wanyonge hadi pale tutakapokubali hatia yetu mbele za Mungu; taabu hii inatupeleka kwa yule pekee anayeweza kutusamehe dhambi zetu. Kati ya mambo yote tunayohitaji ili kubaki karibu na Mungu, lililo kuu zaidi ni dhamiri ambayo inaweza kufahamishwa kwa urahisi kuhusu kile ambacho Mungu anataka na nia yake ya kutuonyesha rehema ikiwa tu tutakuwa tayari kukiri kosa tulilofanya na kuja kwake ili kupokea rehema yake tena. Asante Mungu kwa baraka za huzuni! Baada ya kutamka na/au kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (katika kiambatisho), sali sala ifuatayo: Mungu wa Milele, Baba yetu, asante kwa nguvu ya uzima ya Neno la Mungu, na jinsi Roho wako Mtakatifu anavyoweka Neno hilo ndani ya mioyo yetu. Asante kwa nguvu yake ya uthibitisho wa Neno lako, unaotufunulia sisi kutostahili kwetu na pia rehema yako kuu. Uko tayari kuwasamehe wale wanaokujia kwa mioyo iliyovunjika na wazi mbele zako. Utupe neema leo ya kusimama tukihitaji nguvu ya uthibitisho ya Neno lako, na nguvu ya utakaso ya damu ya Mwanao. Kwako, wewe peke yako, ndiko inakopatikana rehema na msamaha na neema. Utukufu uwe kwako, katika Jina la thamani la Yesu, Amina!
ukurasa 183 2
2
Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi
ukurasa 183 3
Made with FlippingBook flipbook maker