Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

/ 4 5

U O N G O F U & W I T O

Bwana Mungu, Baba wa mbinguni, ambaye kwako tunapokea mema yote kwa wingi, na ambaye kwa uweza wako tunalindwa kila siku na maovu yote kwa neema, utusaidie, tunakuomba, tuchukue karama hizi zote kwa njia ya Roho wako Mtakatifu kwa ukamilifu wa moyo na imani ya kweli, ili tuweze kushukuru na kusifu wema wako na rehema zako; kwa Yesu Kristo Mwanao na Bwana wetu. Amina. ~ Martin Luther. Devotions and Prayers of Martin Luther . Trans. Andrew Kosten. Grand Rapids: Baker Book House, 1965. Uk. 77.

Weka kando vitabu na madokezo yako, kusanya mawazo na tafakari zako, na ufanye jaribio la somo la 1, Neno Linaloumba .

Jaribio ukurasa 184  4

2

Mazoezi ya Kukariri Maandiko

Fanya mazoezi pamoja na mwanafunzi mwenzako, andika na/au nukuu kwa kutamka andiko la kukumbuka ulilopewa katika kipindi kilichopita: 2 Petro 1:19-21.

ukurasa 184  5

Kusanya muhtasari wako wa kazi ya usomaji ya wiki ililopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache kuhusu mambo muhimu uliyoyaona katika vitabu ulivyoelekezwa kusoma, yaani hoja kuu ambazo waandishi walikusudia kuziwasilisha (taz. Fomu ya Ripoti ya Usomaji).

Kazi za Kukusanya

MIFANO YA REJEA

Dini ya Kweli na Isimame, Tafadhali!

Katika darasa la falsafa katika chuo kikuu kilichopo katika eneo lako, mmoja wa wazee wa kanisa lako alikumbana na wazo la “uhusiano wa kitamaduni.” Wazo hili linadai kwamba tamaduni zote ni sawa, na mifumo yake yote mbalimbali ya imani, mawazo ya kidini, na kanuni za kimaadili ina uhalali unaolingana. Wazo hili limemsumbua kiongozi wa kanisa, ambaye anaamini kwamba Yesu Kristo kwa namna fulani ni wa kipekee na mkuu juu na zaidi ya mifumo na mawazo mengine yote ya kidini. Je, mzee huyu anapaswa kuuelewaje mtazamo huu mahususi wa “uhusiano wa kitamaduni,” na wazo hili linahusiana vipi na dai la Biblia kwamba ufunuo wa Mungu katika Yesu kwa namna fulani ni mkuu kuliko imani na dhana nyingine yoyote? (taz. Ebr. 1:1-2).

1

ukurasa 184  6

Made with FlippingBook flipbook maker