Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
4 6 /
U O N G O F U & W I T O
Nyimbo Zipi Hasa ni “Nyimbo za Sayuni”?
Mjadala mzito unazuka miongoni mwa washirika wa kikundi cha vijana kuhusu aina ya muziki unaokubalika kwa vijana Wakristo kusikiliza. Yote yalianza wakati mmoja wa vijana alipoleta CD ya mmoja wa wasanii wa muziki wa kufoka maarufu kama “rap” wanayempenda sana ili kuicheza kwenye kikundi cha vijana, na baadhi ya watoto walipinga aina fulani ya mambo ambayo msanii huyo aliyataja katika nyimbo zake. Kijana aliyeleta muziki huo, ambaye ni Mkristo anayekua na mwenye kumpenda Mungu sana, aliumizwa sana na mabishano hayo, akiamini kwamba ni muhimu kuelewa kinachoendelea ulimwenguni ikiwa wanataka kuwa mashahidi wazuri kwa marafiki zao waliopotea. Wengine, wenye kumpenda Mungu pia, walipinga hoja hiyo wakidai kwamba aina hii ya muziki si ya kimungu; walionelea kwamba maneno yaliyojaa katika nyimbo hizo kuhusu jeuri na maumivu na mapambano si ya kutia moyo bali yanahuzunisha. Kila upande unaonekana kuamini kwa uzito uleule juu ya umuhimu wa suala hilo na kushikilia msimamo wa “upande” wao kuwa wa kweli. Je, ni ipi njia bora ya kutatua mgogoro na msuguano huu kati ya pande hizi zinazopingana kuhusu suala hili la muziki? Hivi majuzi, watu wa kikundi kidogo kinachojifunza kuhusuMambo ya Mwisho na Ujio wa Pili wa Yesu Kristo walianza kusoma hukumu mbalimbali zinazohusiana na nyakati za mwisho. Kwa mmoja wa akina dada katika kikundi, somo hilo limesababisha mfadhaiko mwingi ndani yake na kuchanganyikiwa, hasa katika jambo moja—wazo la Mungu kuwahukumu wale ambao hawajawahi kusikia kuhusu Kristo. Akilini mwake, wazo la kwamba Mungu atawahukumu watu wote, hata wale ambao hawajapata nafasi ya kusikia kumhusu Yesu na upendo wake, linachukiza. “Mungu hawezi kufanya hivyo—hilo halingekuwa jambo la haki kuwahukumu watu ambao, bila kukusudia, kamwe hawajapata kumjua Mungu. Wataishia kuhukumiwa na Mungu na hata kwenda kuzimu kwa sababu tu hakuna mtu aliyewahi kuwaambia kuhusu Bwana.” Kwa wengine katika somo, suala si Mungu kuwa au kutokuwa na upendeleo bali ni utakatifu wake. Wanadai kwamba ikiwa Mungu hatawahukumu wote kulingana na kiwango alichoweka (yaani, imani katika Kristo) atakuwa amevunja uadilifu wake mwenyewe, kwa maana amesema kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa (yaani, imani katika Kristo taz. Rum. 10:9-10). Japokuwa wameendelea kulijadili kwa uwazi, hawajaweza kusuluhisha suala hilo. Wafanye nini? Sio Haki Kabisa!
2
2
3
Made with FlippingBook flipbook maker