Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

/ 4 7

U O N G O F U & W I T O

Neno Linalothibitisha Sehemu ya 1

YALIYOMO

Mch. Dkt. Don L. Davis

Katika sehemu hii, tutachunguza jinsi Neno la Mungu, kama chombo cha Roho Mtakatifu, linavyouthibitishia ulimwengu kuhusu dhambi, haki, na hukumu. Kuhusiana na dhambi, Neno la Mungu hututhibitishia kwa habari ya kutotii kwetu sheria ya Mungu na kushindwa kuoanisha maisha yetu na tabia na matakwa yake matakatifu. Kuhusiana na haki, Neno la Mungu linafunua umbali kati ya Bwana kama Mungu mwenye haki isiyo na kikomo na haki yetu wenyewe, ambayo haikubaliki kwake. Hatimaye, tutalitazama Neno la Mungu kuhusiana na mafundisho yake juu ya hukumu, na kujifunza kuhusu nia ya Mungu ya kuhukumu viumbe vyote kwa msingi wa vigezo vya haki yake, na utii wao kwa vigezo hivyo. Lengo letu la sehemu hii ya kwanza ya Neno Linalothibitisha ni kukuwezesha kuona kwamba: • Neno la Mungu ndilo Neno linalothibitisha kuhusu dhambi, haki, na hukumu. • Kati ya njia zote tunazoweza kumwelewa Mungu na kuielewa kazi yake, ni Neno la Mungu katika Maandiko linalotuwezesha kuielewa dhambi – kwamba ni ya ulimwengu wote katika upeo wake na ina asili ya uharibifu. • Sheria ya Mungu hututhibitishia kwa habari ya dhambi zetu, ikifunua umbali kati ya matendo na nia zetu na matakwa matakatifu ya Mungu. • Neno la Mungu huthibitisha kuhusu haki, likiweka wazi kupungua kwetu katika kushika Sheria ya Mungu, na kuifunua haki ya Mungu kwa imani kupitia kifo na ufufuo wa Yesu Kristo. • Neno la Mungu linathibitisha kuhusu hukumu, likifunua nia ya Mungu ya kuhukumu viumbe vyote kila mahali, na hukumu yake inayokuja juu ya Israeli na mataifa, juu ya Kanisa, juu ya Shetani na malaika zake, na wafu wote waovu.

Muhtasari wa Sehemu ya 1

2

Made with FlippingBook flipbook maker