Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

/ 5

U O N G O F U & W I T O

Utangulizi wa Moduli

Salamu, wapendwa marafiki, katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Kama wanafunzi wa Yesu Kristo, tunathibitisha imani yetu ya kina katika nguvu ya Neno la Mungu linaloumba, linalothibitisha, linalogeuza na kuita watu katika utumishi. Ili kuelewa baraka ya ajabu ya uongofu na wito, tutahitaji kutathmini kwa kina nafasi ya Neno la Mungu katika Kanisa. Somo letu la kwanza, Neno Linaloumba , linachunguza asili ya Maandiko Matakatifu kama Neno la Mungu. Tutaona kwamba uadilifu kamili wa Mungu mwenyewe ni msingi wa kuaminika kwa Maandiko kusikoweza kutiliwa shaka. Zaidi ya hayo, tutaangazia jinsi Mungu alivyoumba ulimwengu kupitia Neno lake, na jinsi anavyojihusianisha kikamilifu na Neno katika Yesu Kristo. Sisi kama vyombo ambavyo Roho Mtakatifu hutumia kuumba maisha mapya ndani ya wale wanaoamini, tunathibitisha kuwa sisi ni wanafunzi wa kudumu wa Neno la Yesu. Kama washirika wa Kanisa, tunapokea Neno pamoja katika kusanyiko, Neno lile lile linalotupatia kusudi kuu la ulimwengu ulioumbwa, ambalo ni utukufu wa Mwenyezi Mungu. Katika somo linalofuata, Neno Linalothibitisha , tutaangalia jinsi Neno la Mungu linavyothibitisha juu ya dhambi, haki, na hukumu. Neno linafundisha kwamba dhambi imeenea katika ulimwengu wote na ina asili ya uharibifu. Neno la Mungu pia huthibitisha kuhusu haki, likiifunua haki kamilifu ya Mungu na kutotosheleza kwetu kimaadili. Na, linathibitisha kwa habari ya hukumu, likifundisha kwamba Mungu atawahukumu kwa hukumu yake ya haki Israeli na mataifa, Kanisa, Shetani na malaika zake, na waovu wote waliokufa. Neno la Mungu pia hututhibitishia juu ya kweli—ya Yesu Kristo, Ufalme wa Mungu, na uadilifu wa Neno lake kupitia wajumbe wake, manabii na Mitume. Somo la tatu, Neno Linalogeuza , linazingatia nguvu ya Neno la Mungu kuleta maisha mapya ndani ya mwamini. Neno hili linalobadilisha kwa maneno mengine ni Injili ya Yesu; ni habari njema ya wokovu ambayo inatufanya “tuzaliwe mara ya pili,” tupitie tendo la kuoshwa kwa kuzaliwa upya, na kufanywa upya na Roho Mtakatifu. Neno huzaa ndani yetu sisi tunaoamini ishara thabiti za uwezo wa Mungu wa kufanya upya. Neno hili hili ambalo huzalisha maisha mapya, pia hututegemeza, hutupatia lishe ya kiroho, husababisha ukuaji wetu, na hutuwezesha kujilinda dhidi ya uongo wa shetani. Hatimaye, somo la nne, Neno Linaloita , linachunguza dhana ya ( metanoia ), yaani, toba kwa Mungu, na imani (pistis ). Imani katika Yesu Kristo ndiyo njia ambayo

Made with FlippingBook flipbook maker