Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

/ 6 9

U O N G O F U & W I T O

(kutubu dhambi na kumgeukia Mungu kwa njia ya Yesu Kristo) na pistis , (yaani imani ambayo kupitia kwayo Mungu humwokoa na kumkomboa mtu kutokana na adhabu, nguvu, na uwepo wa dhambi). Neno hili linalogeuza huzaa ishara za ndani za maisha mapya ya kiroho ndani ya mwamini, zikijumuisha kumjua Mungu kama Baba wa mbinguni, uzoefu mpya wa maombi, uwazi kwa Neno la Mungu, na nia ya kufuata maongozi ya ndani ya sauti ya Yesu. Tutaona zaidi jinsi ishara za nje zinavyoonekana, zikijumuisha utambulisho na ushirika pamoja na watu wa Mungu, udhihirisho wa tabia na mtindo mpya wa maisha yanayomfanania Kristo, upendo kwa waamini wengine, na hamu ya kuona waliopotea wakivutwa kwa Kristo.

2

Made with FlippingBook flipbook maker