Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
6 8 /
U O N G O F U & W I T O
unavyoweza kumwamini Mungu kwa ajili ya Neno lake (Maandiko) kupata nafasi na nguvu kubwa zaidi ya uthibitisho katika maisha yako?
Somo hili limesisitiza uhusiano wa moja kwa moja kati ya Neno la Mungu na Roho wa Mungu. Ili Neno la Mungu liwe na mamlaka kamili maishani mwetu, ni lazima tumwombe Mungu atufundishe Neno lake kwa Roho wake, aithibitishie mioyo yetu juu ya dhambi yoyote, kiburi, upumbavu na upinzani unaoweza kuwa ndani yetu na kisha, kwamba aruhusu Neno lilelile lenye nguvu liguse maisha ya wale tunaowaombea na kuwahudumia. Usidharau kamwe uwezo wa Neno la Mungu kuyeyusha moyo ulio na nta au kumgeuza mtu kutoka katika njia yake uharibifu na kumgeukia Bwana. Omba kwamba Mungu akupe uhakikisho zaidi kuhusu uvuvio, usahihi (yaani, kutokuwa na makosa) na uwezo mkuu wa Neno lake. Ni kadiri tu tunavyoishi nguvu ya Neno la Mungu inayothibitisha ndipo tutakapoelewa uwezo wake wa kuponya, kubadilisha, na kuangazia mioyo ya wengine.
Ushauri na Maombi
ukurasa 189 19
2
MAZOEZI
Yohana16:7-11
Kukariri Maandiko
Ili kujiandaa kwa ajili ya kipindi, tafadhali tembelea www.tumi.org/books kupata kazi ya usomaji ya wiki ijayo, au muulize Mkufunzi wako.
Kazi ya Usomaji
Kwa mara nyingine tena, hakikisha kwamba umesoma vizuri kuhusu kazi zilizo hapo juu, na kama wiki iliyopita, ziandikie muhtasari mfupi na ulete muhtasari huo darasani wiki ijayo (tafadhali angalia “Fomu ya Ripoti ya Usomaji” mwishoni mwa somo hili). Pia, sasa ni wakati wa kuanza kufikiria kuhusu mwelekeo wa kazi yako ya mafunzo ya huduma kwa vitendo, na pia kuamua ni kifungu gani cha Maandiko utakachochagua kwa ajili ya kazi yako ya ufafanuzi Maandiko (eksejesia). Usichelewe kufanya maamuzi kuhusu kazi yako ya huduma kadhalika na ile ya eksejesia. Kadiri utakavyofanya maamuzi haraka kuhusu kile unachokusudia kufanya, ndivyo utakavyokuwa na muda wa kutosha kujiandaa na kufanya kazi zilizo bora zaidi.
Kazi Nyingine
Somo letu linalofuata, somo la tatu la moduli yetu ya Uongofu na Wito, linaitwa, “ Neno Lililogeuza .” Katika kipindi chetu kijacho tutagundua jinsi ambavyo Injili ya Yesu Kristo ni Neno lile linalogeuza, ambalo linaongoza kwenye metanoia ,
Kuelekea Somom Linalofuata
Made with FlippingBook flipbook maker