Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

/ 6 7

U O N G O F U & W I T O

Neno la Mungu linathibitisha juu ya dhambi, haki, hukumu na kweli. Kuhusiana na dhambi, Neno linafundisha kwamba dhambi ni ya ulimwengu wote katika upeo wake na ina asili ya kuwapotosha wanadamu. Kuhusiana na haki, Neno la Mungu linashuhudia juu ya haki kamilifu ya Mungu, na zawadi yake ya haki kwa njia ya neema kwa waamini kupitia kifo na haki ya Yesu Kristo. Kuhusiana na hukumu, Mungu atawahukumu watu wote kulingana na matendo yao. Hukumu yake ya mwisho itakuwa pana, ikijumuisha Israeli na mataifa, Kanisa, Shetani na malaika zake, pamoja na wale waliokufa ambao hawakumwamini Yesu Kristo. Hatimaye, Neno la Mungu hutuhakikishia kuhusu kweli. Yesu Kristo ndiye mada kuu ya Maandiko, na mpango wa ufalme wa Mungu kupitia kwa Ibrahimu ndio msingi wa kazi ya Mungu. Ukweli na usahihi wa Neno unatokana na huduma ya manabii, Mitume, na Yesu Kristo, na kuifanya Biblia yetu kuwa ya kuaminika kabisa kwa masuala yote ya imani na mwenendo (maisha). Iwapo ungependa kufuatilia baadhi ya mawazo ya somo hili la Neno Linalothibitisha , unaweza kujaribu vitabu vifuatavyo: Pinnock, Clark H. Biblical Revelation: Foundation of Christian Theology . Chicago: Moody Press, 1971. Hapa ndipo unapopata fursa ya kuchunguza matumizi mahususi, ya moja kwa moja ya maarifa ya somo katika hali yako halisi ya kiutendaji ya huduma. Nguvu ya uthibithisho ya Neno la Mungu inafanya kazi katika maisha yetu yote, na labda inawezekana kuna eneo mahususi la kazi yako katika kanisa lako, au katika huduma yako kwa niaba ya kanisa lako ambalo limeguswa kipekee na somo hili. Kwa kuanzia, vipi kuhusu maisha yako mwenyewe—Je, Neno la Mungu linakuthibitishia kuhusu kweli? Je, kuna eneo katika maisha yako ambalo kweli ya Mungu inahitaji kupewa nafasi kubwa na ya wazi zaidi? Je, unalielewa Neno la Mungu zaidi na zaidi, na je, linazalisha ndani yako aina ya mitazamo na mielekeo inayopasa? Vipi kuhusu wale unaowahudumia—je, wanapata ufahamu zaidi na zaidi wa Neno la Mungu? Je, unahitaji kutafuta neema ya Bwana kwa ajili yao – kwa maana ya kwamba wanahitaji neno la uthibitisho katika baadhi ya maeneo ya maisha yao? Je, ni nini hasa ambacho Roho Mtakatifu anazungumza na wewe kuhusiana na “Neno linalothibitisha,” kwa ajili yako, familia yako, kanisa lako, huduma yako? Ni hali gani hasa inakuja akilini unapofikiria kuhusu jinsi Smart, J. D. The Interpretation of Scripture . London: SCM press, 1961. Young, E. J. Thy Word is Truth . London: Banner of Truth, 1963.

Marejeo ya Tasnifu ya Somo

2

Nyenzo na Bibliografia

Kuhusianisha Somo na Huduma

ukurasa 188  18

Made with FlippingBook flipbook maker