Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
6 6 /
U O N G O F U & W I T O
anayeweza kudai kwamba kitu fulani ni dhambi, kwa kuwa «dhambi» ina maana tu ndani ya muktadha wa kikundi husika cha kidini. Je, ungeweza kumshauri nini kijana huyu mfanyakazi wa kijamii kuhusiana na dhana hii ya «dhambi»?
Haki ya Nani ni Haki Zaidi?
Baada ya mazungumzo marefu na yenye mvutano na Shahidi wa Yehova, mmoja wa washirika wa kanisa lako alijikuta akiangukia kwenye mojawapo ya hoja zilizotolewa dhidi ya Kanisa. Kwa kulinganisha kiwango cha ubora wa maisha ya Shahidi wa Yehova na waenda-kanisani wa kawaida, Shahidi huyo alidai kwamba “Ingawa suala la haki na uadilifu linazungumzwa sana kanisani, kwa sehemu kubwa, unaweza kufanya chochote unachotaka na bado ukaendelea kama kawaida. Kwa hakika, niliwahi kuhudhuria kanisa ambalo wanamuziki walijihusisha na zinaa, shemasi mmoja alilipuka na kumzomea mchungaji katika kikao cha kazi, na mhudumu wa vijana akatengana na mke wake. Hata hivyo, hakuna mtu aliyesema chochote kuhusu mambo hayo. Tangu nimekuwa Shahidi wa Yehova, hata hivyo, kwa kweli tunaishi kwa uadilifu kati yetu, na hatuwezi kumvumilia yeyote anayeishi isivyo haki.” Mshirika wa kanisa lako alijua hali kama hizi, na alijisikia kunyong’onyeshwa na hoja hizo. Je, utamshauri vipi kujibu hoja za namna hii wakati mwingine endapo atakutana na madai kama hayo kuhusu haki? Hivi majuzi, umeteuliwa kuwa Msimamizi wa Shule ya Jumapili ya kanisa, na uko katika mchakato wa kuchagua walimu wa masomo mbalimbali unayotoa kulingana na umri wa wanafunzi. Umeangalia nyuma katika mwaka uliopita katika nusu ya masomo yaliyofundishwa na umegundua kuwa hakuna somo moja ambalo ni la msingi linalotiliwa mkazo na kuzingatiwa katika madarasa. Kumekuwa mijadala mbalimbali kuhusu kila aina ya masuala na mada katika madarasa ya makundi mbalimbali kulingana na umri, na hakuna hata kundi moja linaloonekana kuwa na hamu sana ya kuzingatia masomo ya kitheolojia. Walimu wengi wamekuwa wakichagua mada kama vile, “Namna ya Kusimamia Pesa Zako,” au “Kuishi Maisha Safi Mbele za Mungu,” au “Namna ya Kuwa na Maisha Bora ya Maombi.” Una wasiwasi kwamba hakuna mafundisho ya kutosha na ya kina yanayotolewa kuhusu Yesu Kristo na kazi yake, na unataka kuwa na mkutano na walimu ili kuzungumzia jinsi ya kufanya hivyo. Je, unaweza kukabiliana vipi na suala hili pamoja na walimu wako, bila kuwajengea hisia ya hatia juu ya mada na mbinu nyingine walizozoea? Kufanya Jambo Kuu Libaki Kuwa Jambo Kuu
3
2
4
Made with FlippingBook flipbook maker