Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

/ 7 3

U O N G O F U & W I T O

Neno Linalogeuza

S O M O L A 3

ukurasa 191  1

Karibu katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Unapomaliza kazi yako katika moduli hii, tunaamini kwamba utaweza kuelewa, kueleza, na kutetea ukweli kwamba: • Neno linalogeuza kwa lugha nyingine ni habari njema ya wokovu kwa imani katika Yesu Kristo. Injili ya Yesu Kristo ndilo Neno linalogeuza. • Neno hili lenye nguvu hutuongoza vyema kwenye metanoia , yaani, toba ya dhambi na kumgeukia Mungu katika Yesu Kristo. • Neno hili ambalo hufanya kazi kwa ufanisi kuleta toba ( metanoia) kwa ajili ya wokovu, hufanya kazi kwa nguvu ileile kuzalisha imani ( pistis ) ndani ya mwamini. Imani hii humwokoa na kumkomboa mwamini kutokana na adhabu, nguvu, na uwepo wa dhambi. • Neno la Mungu, mara linapoamilishwa na toba na imani, huzalisha ishara zinazothibitisha msamaha wa Mungu na uwepo wa nguvu za Roho Mtakatifu katika maisha ya mwamini. • Kwa ndani, mwamini anaonyesha ishara za maisha mapya katika Yesu Kristo, zikijumuisha kumjua Mungu kama Baba wa mbinguni, uzoefu mpya wa maombi, uwazi kwa Neno la Mungu, na nia ya kufuata uongozi wa ndani wa sauti ya Yesu. • Kwa nje, na kwa njia inayolingana, Neno ligeuzalo linatoa ishara za nje zikijumuisha mambo kama vile kujitambulisha na kuwa na ushirika pamoja na watu wa Mungu, udhihirisho wa tabia mpya na mtindo mpya wa maisha kama wa Kristo, upendo kwa waamini wengine, na hamu ya kuona waliopotea wakirudi kwa Kristo.

Malengo ya Somo

3

Lazima Uzaliwe Mara Ya Pili

Ibada

Soma Yohana 3:1-21 . Kati ya maajabu yote makuu ya mafundisho ya Yesu kuhusu ufalme tunayojifunza na kufurahia, labda hakuna inayogusa kama mafundisho yake kuhusu hitaji la kuzaliwa kutoka juu – kuzaliwa mara ya pili. Uzoefu wa uzazi unatupatia mwanga wa ufahamu wa rohoni. Tendo la kuzaliwa kwa mtoto mdogo ulimwenguni, marafiki na familia wakipokea kwa furaha maisha haya mapya ulimwenguni, katika ulimwengu wao, ni wakati wa ajabu na wa furaha. Yesu alitumia

ukurasa 191  2

Made with FlippingBook flipbook maker